Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, September 2, 2011

Mkandarasi apewa siku 42 kukamilisha soko

KAMPUNI ya Tanzania Bulding works Limitted ya Dar es Salaam imepewa
siku 42 inayojenga soko jipya la Mwanjelwa jijini hapa kuhakikisha
ujenzi wa soko hilio unakamilika.

Halmashauri ya jiji la Mbeya imetoa agizo hilo baada ya kuona tarehe
ya kukabidhiwa kwa soko imefika lakini ujenzi bado haujakamilika
ambapo mkataba unaonesha ulipaswa kukamilika agosti 24

January 25,2010 serikali ilimpa miezi 18 mkandarasi huyo kuhakikisha
soko hilo linakamilika na kukabidhiwa kwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya
Agosti 24, mwaka huu  lakini kutokana na sababu zinazoelezwa kuwa za
kiufundi  soko hilo limeshindwa kukamilika kwa wakati muafaka.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Juma Idd amesema muda wa ziada
uliotolewa kwa mkandarasi Mohamedy Hashed unatosheleza kukamilisha
ujenzi uliobakia baada ya miezi 18 ya mkataba kumalizika huku ujenzi
ukiwa bado.

Idd amesema leo (Agost 30) mbele ya waandishi wa habari kuwa agizo
lililotolewa na halmashauri si la kukamilisha ujenzi pekee na
kukabidhi soko hilo bali viwango vitazingatiwa

Ujenzi wa soko hilo jipya unagharamiwa na halmashauri ya jiji ikiwa ni
mkopo wa shilingi bilioni 13, kutoka Benki ya CRDB  ambapo kati ya
fedha hizo shilingi bilioni moja zilitumika kulipa fidia kwa wamiliki
31wa nyumba katika eneo husika.

No comments:

Post a Comment