Hatua ya vijana walioko mashuleni na vyuoni kujiingiza
katika siasa imetajwa kuwa ugonjwa mbaya unaohatarisha taaluma nchini pamoja na
mustakabali wa maisha ya watanzania miaka michache ijayo.
Ili kuepuka na balaa linaloweza kuikumba nchi badae
vijana hao wametahadharishwa kutojiuhusisha na siasa na badala yake waelekeze
nguvu zao kwenye masomo ili kuinua kiwango chao cha Taaluma.
Mwenyekiti wa Chama cha Kuweka na kukopa (Saccos) cha
Walimu wa shule za Sekondari wilayani Mbeya, Frank Phiri ameyasema hayo kwenye
mahafari ya pili ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Itebwa ambapo
jumla ya wanafunzi 86 wamehitimu.
Amesema wanafunzi wanapaswa kutambua kuwa viongozi
wakisiasa wakongwe wanaowashabikia hivi sasa walijiingiza katika siasa hiyo
baada ya kutoka masomoni na si wakiwa masomoni na ndiyo maana taaluma zao
zinaonekana kuwa nzuri.
Awali Mwalimu Mkuu wa shule, Mpege Mwamkota amesema shule hiyo
inakusudia kuboresha huduma za hosteli ili
kukabiliana na changamoto ya wanafunzi wa kike kukatisha masomo kutokana na kupata
mimba.
No comments:
Post a Comment