Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, September 23, 2011

Kikao kuwapika viongozi wa halmashauri Mbeya


MAZUNGUMZO YA KATIBU TAWALA MKOA BIBI BEATHA O. SWAI KATIKA KUELEZA MADHUMUNI YA MAFUNZO YA KILIMO TAREHE 22 -23 SEPTEMBA, 2011 MKOANI MBEYA.
*      Wazo la kuendesha mafunzo ya uvuvi, nyuki, samaki, Stakabadhi ya Mazao Ghalani na Huduma za Ugani kwa viongozi na watalaamu  yametokana na mawazo yafuatayo:-

i.                    Mkoa haujafikia lengo la kuzalisha tani 4,459,995
ii.                 Mfumo wa Stakabadhi ya Mazao Ghalani haujaeleweka vema kwa wadau.
iii.               Sekta za uvuvi, nyuki na samaki hazijaendelezwa ipasavyo licha ya Mkoa kuwa na fursa kubwa ya kuendeleza Sekta hizi.
iv.               Mfumo wa uwajibikaji katika kusimamia kilimo unapashwa kuboresha ili kufikia malengo yaliyowekwa.
v.                  Pia kutekeleza maazimio yaliyofikiwa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika “Retreat” ya Homboro Julai 2011 pamoja na .”Retreat” ya Viongozi wa ngazi ya Mkoa na Wilaya iliyofanyika tarehe 18 Agosti, 2011 Mkoani Mbeya.

*      Mafunzo haya ya siku mbili (22-23 Septemba, 2011) yatatolewa na wawezeshaji ifuatavyo:-
i.                    Bw. Shangwe Twamala – Katibu Tawala Msaidizi – Uchumi kutoka RS Mtwara ambaye atatoa mada za:
a.      Mfumo wa Stakabadhi ya Mazao Ghalani
b.      Mfumo wa usimamizi wa Huduma za Ugani
ii.                 Bw. Edwin Meela – Afisa Nyuki – HW Manyoni ambaye atatoa mada ya ufugaji bora wa nyuki
iii.               Bw. Walece Z. Masha – Afisa Uvuvi – RS Ruvuma ambaye atatoa mada kuhusu ufugaji bora wa samaki, na
iv.               Bw. Jaliwa A. Ntibiyoboka -(Afisa Ushirika  HW Mpanda ambaye atatoa mada za:-
a.      Matumizi ya Daftari la Kilimo na
b.      Dhana ya Waganikazi kutika Huduma za Ugani

*      Washiriki wa mafunzo haya wamechaguliwa kwa makini kwa sababu aidha ni Wasimamizi na wafuatiliaji (DC, DED, M/kiti HW, M/Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira ya HW) au ni watekelezaji (wataalamu na wakulima). Hivyo mafunzo haya yatawafaa.

*      Matarajio kutokana na mafunzo haya ni kwamba:-
        i.            Washiriki wote kupata uelewa wa pamoja kuhusu masuala ya ufugaji bora na wa kibiashara wa nyuki na samaki, matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi ya Mazao Ghalani na mfumo bora wa Huduma za Ugani kwa wakulima na wafugaji.
     ii.            Kupata uzoefu wa utekelezaji wa maeneo hayo kutoka kwa wawezeshaji.
   iii.            Kupata mawazo mbalimbali kutoka kwa washiriki kuhusu namna ya kuwa na mikakati ya kuendeleza sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, nyuki pamoja Mfumo wa Stakabadhi ya Mazap Ghalani na Huduma za Ugani kwa wakulima na kufikia makubaliano ya utekelezaji katika Mkoa wetu.

*      Mhe. Mwenyekiti baada ya maelezo haya ya utangulizi naomba nikukaribishe rasmi ufungue mafunzo haya.

No comments:

Post a Comment