Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, September 25, 2011

14 wafa katika ajali ya fuso,zaidi ya 40 wajeruhiwa


Watu 14 wamekufa na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa  baada ya lori walilokuwa wakisafiria kutoka mnadani katika kijiji cha Mbuyuni Wilayani  Chunya kupinduka katika eneo la Mlima Msangamwelu barabara ya Mbalizi-Chunya.

Ajali hiyo imetokea jana Septemba 24 mwaka huu majira ya saa 12:00 jioni katika eneo la Mlima Msangamwelu ambapo mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo, Eden Sanga amesema gali hilo aina ya fuso lililokuwa limebeba abiria pamoja na mizigo lilishindwa kupanda mlima na kupinduka kutokana na kufeli kwa breki.

Sanga amesema kulikuwa na magari mawili yameongozana ambapo wote walikuwa wanatokea mnadani na kwamba fuso walilokuwa wamepanda wao lilifanikiwa kupanda mlima huo bila matatizo lakini gari la wenzao lilishindwa kupanda mlima huo na kupinduka.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Anacret Malindisa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, ambapo alisema watu 11 walifariki papo hapo mara baada ya ajali hiyo kutokea na wengine watatu walifariki jana asubuhi wakati wakipatiwa matibabu katika Hospitali Teule ya Ifisi iliyopo Mbalizi.

Amesema watu hao walikuwa wanasafiri katika lori aina ya fuso lenye namba za usajili T 532 AJF lililokuwa likitokea Mbuyuni Wilayani Chunya ambapo lilikuwa limebeba mizigo na watu ambao  walikuwa wakitoka mdani.

Amewataja watu waliokufa katika ajali hiyo ambao wametambulika kwa jina moja moja kuwa ni  Exzavery, Kaloli, Lembo, Masai, Kashinje,  Noa,mama Anna Ugalahenga, Mwakalasya, Meshack na Mwakilasa ambvao miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya,

Hata hivyo Malindisa amesema kuwa  watu wengine watatu waliofariki leo asubihi katika hospitali  teuleya ifisi  bado majina yao hayajatambuliwa.Aidha alisema uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo bado unaendelea na kwamba taarifa kamili itatolewa baadae.

No comments:

Post a Comment