JAMII mkoani Mbeya imehimizwa kujitolea kwenye uttafutaji wa suluhu za
changamoto zilizopo kwenye maeneo yao badala ya kubaki wakisubiri serikali
kutekeleza kila jambo.
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kata ya Iwambi
jijini Mbeya walitoa hamasa hiyo kwenye shughuli ya ukarabati wa jengo la
darasa la Kidato cha kwanza B lililopo katika shule ya sekondari ya Iwambi
ambapo wanachama wa chama hicho wameamua kujitolea kulikarabati.
Mwenyekiti wa CCM kata ya Iwambi Cyprian Gamba amesema
wamehamasika kukarabati jengo hilo ikiwa ni ahadai waliyoitoa kwenye ziara ya
Waziri mkuu Mizengo Pinda alipotembelea shule hiyo kwaajili ya kuzindua
maabara.
Akizungumza na Lyamba Lya Mfipa Mapema leo shuleni hapo,Gamba amesema
wanachama wa CCM kata ya Iwambi wameguswa na kilio cha wanafunzi na walimu
shuleni hapo na kuona haja ya kukarabati moja ya majengo yaliyo na hali mbaya.
Amesema ni wakati kwa jamii kubadili mrtazamo kwa
kushiriki kutatua changamoto ndogo ndogo kwenye maeneo yao badala ya kuiachia
serikali kutekeleza kila jambo.
Kwa upande wake katibu wa CCM kata ya Iwambi Geoge
Nyirenda amesema wameamua kuchanga michango na kwa kuanza wamefanikiwa
kukusanya kiasi cha shilingi laki sita na lengo ni kuboresha chumba cha darsa
hilo kuanzia sakafu hadi madirisha.
Nyirenda ameitaka jamii kutouhusisha mchango huo na
harakati za kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu ujao huku akisema huo ni mchango
wa wanaccm katika maendeleo ya kata na ndiyo sababu haujatolewa na mtu mmoja.
No comments:
Post a Comment