MWANAHABARI Gordon Kalulunga
ametangaza nia ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilayani hapa kumpa
nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho akigombea nafasi ya ubunge wa
jimbo la Mbeya vijijini kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Kalulunga alitangaza nia hiyo alipozungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Mahubiri vilivyopo
katika mji mdogo wa Mbalizi wilayani hapa,mkutano uliohudhuriwa pia na wakazi
mbalimbali kutoka ndani na nje ya mji huo.
Akizungumzia nia hiyo,Kalulunga
alisema anawania nafasi ya ubunge wa jimbo hilo kwa lengo la kuwatumikia
wananchi na kamwe si kwaajili ya kupata kinga kwa shughuli zozote zenye maslahi
yake binafsi.
Alisema kwa muda mrefu kumekuwa
na tabia jimboni hapa ya viongozi kujitokeza kugombea nyadhifa mbalimbali
wakilenga kupata nafasi ya kuutumia uongozi kama kinga kwa biashara
wanazofanya.
“Sigombei ili nilinde maslahi
ya shughuli ninazofanya,wala kulinda kabila lolote.Nagombea ili niwatumikie
wakazi wa jimbo la Mbeya vijijini.Tunapowachagua watu wanaotaka kulinda maslahi
yao tutabaki kulalamikia serikali kuwa haituletei maendeleo lakini ukweli ni
kuwa tutakuwa tumewasaidia watu wachache kutimiza malengo yao”
“Wilaya yetu ni wilaya
inayopakana na wilaya karibu zote za mkoa wa Mbeya isipokuwa wilaya za Kyela na
Momba lakini ni wilaya isiyokuwa na hata chuo kimoja kinachotoa walau taaluma
yoyote hata katika ngazi ya cheti.Ni kwa sababu hatujapata viongozi wenye
uchungu na maisha yetu” alisisitiza Kalulunga.
Mwanahabari huyo alisema iwapo
atapewa nafasi na CCM na kuweza kuukwaa ubunge wa jimbo hilo,sambamba na
kutekeeza ilani ya chama hicho,pia kipaumbele chake kikuu ni afya ya jamii
kwanza.
Alisema kwake Afya anaipa
kipaumbele kwakuwa mtu yeyeto aliye na afya njema ataweza kushirikia katika
mikakati mbalimbali ya kujiletea maendeleo yeye binafsi,jamii inayomzunguka na
taifa kwa ujumla.
Alisema endapo Chama chake
kitampitisha na hatimaye kushinda Ubunge katika Jimbo hilo atahakikisha
wananchi wote wanajiunga na mfuko wa bima ya afya kwa ajili ya matibabu kwa
kila kaya kuchangia ili kupunguza adha na gharama kubwa za matibabu.
Aliongeza kuwa akifaniiwa
kuukwaa Ubunge pia atasimamia kuhakikisha Jimbo hilo linapata Chuo cha aina
yoyote kikiwemo Chuo cha ufundi kwa ajili ya vijana kupata elimu jambo
lilatalopunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana.
No comments:
Post a Comment