Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, December 19, 2017

WACHANGIA DAMU KAMA ZAWADI YA CHRISMASS








HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya imeandaa Kampeni ya kukusanya Chupa zaidi ya 100 za Damu kwaajili ya kutoa Zawadi ya Krismasi kwa wagonjwa wenye uhitaji wa Damu wilayani hapa.

Kwa mujibu wa kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbarali,Emanuel Kishimbo zoezi la kukusanya damu lilianza Desemba 3 mwaka huu katika kata ya Ubaruku na tangu ianze inaendelea vizuri kwa watu mbalimbali kujitokeza kuchangia.

Kishimbo alisema pia Desemba 5 watumishi wa Sekta mbalimbali katika halmashauri ya wilaya walijitokeza kuchangia Damu katika zoezi lililofanyika Nje ya Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri kabla ya kuhamishia Nje ya Hospitali ya wilaya.

“Lengo letu ni kuchangia zawadi katika msimu huu wa skukuu.Watu wengi msimu huu wanaandaa zawadi mbalimbali kwa watu wanaowapenda na kuwathamini.Sisi tumeona tuwape thamani watu wanaohitaji kuongezewa damu kwa kuwapa zawadi ya damu zetu.Hawa ni waliopata ajali,akina mama wanaojifungua na pia wagonjwa wengine hususani watoto”

“Wito wangu kwa wananchi ni kuendelea kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili kwa sababu sambamba na zoezi la uchangiaji damu watapata pia faida ya kupima afya zao na kuzielewa kama shinikizo la damu,homa ya ini na kaswende na kujua kundi la damu alilo nalo”alisema Kishimbo.

Kwa Upande wake kaimu Mganga mkuu wa wilaya ya Mbarali,Dk Azael Luvanda alisema alisema kwa mahitaji ya damu kwa mwezi wilayani hapa ni kati ya yuniti 10 hadi yuniti 15 na katika kampeni hiyo kwa kata ya Ubaruku pekee waliweza kukusanya yuniti 50.

Dk Luvanda alisema wagonjwa wanaoongoza kwa mahitaji ya damu ni akina mama wajawazito na watu wanaopata ajari huku pia akisema kwa muda mrefu wamekuwa wakitegemea kupata damu kutoka kwa makundi ya wanafunzi.

No comments:

Post a Comment