SERIKALI ya kijiji cha Luhanga wilaayani Mbarali
imesisitiza kuwa uwekezaji wa kilimo unaolengwa kufanywa na Umoja wa wakulima wa
Luhanga unalenga kuwanufaisha wakazi wa kijiji hicho na haupo kwa maslahi ya
watu binafsi.
Uongozi wa kijiji hicho umesema makubaliano ya
mkataba na umoja huo ni pamoja na umoja kutekeleza mambo makuu matatu ikiwemo
kujenga ofisi ya kisasa ya kijiji,kuleta maji kijijini hapo kwaajili ya
matumizi ya kilimo pamoja na kulipia ardhi waliyopewa kwaajili ya shughuli zao.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Muhamed Msonsa alisema
jana kuwa umoja huo utapaswa kulipa shilingi 5000 kwa kila hekari moja ya eneo
walilopewa na kijiji hivyo kijiji kila mwaka kitakuwa kikikusanya jumla ya
shilingi milioni 62 kwa hekari 5000 zilizotolewa.
Kwa upande wa afisa mtendaji wa kata ya Luhanga
Aloyce Joseph alisema wapo wanasiasa wanaoonekana kuingilia kati uwekezaji huo
na kuwalaghai wananchi kuwa kilichofanyika ni unyang’anyi wa ardhi hali ambayo
imeonekana kuwagawa wanakijiji katika makundi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya
ya Mbarali George Kagomba alisema uwekezaji wa Umoja huo utakinufaisha kijiji
kwani kabla hata ya kuanza kwa shughuli husuika tayari umoja huo umeonesha nia
kwa kuanza kuwasaidia wanakijiji kutatua changamoto mbalimbali.
No comments:
Post a Comment