Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, May 20, 2017

BODI,KAMATI ZA SHULE MBEYA ZAAGIZWA KUSIMAMIA MAJUKUMU YAKE

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza kwenye Kongamano la Elimu lililowakutanisha wadau wa sekta hiyo wilayani Kyela.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Dokta Hunter Mwakifuna akizungumza jambo kwa wadau wa Elimu kwenye mdahalo.
Wadau wa Sekta ya Elimu wilayani Kyela mkoani Mbeya wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa mkoa huo,Amos Makalla kwenye Kongamano la Elimu.



Diwani wa kata ya Itunge wilayani Kyela,Cecilia Jimmy akichangia mjadala wa Elimu katika Kongamano la Sekta ya Elimu lililofanyika mjini Kyela.
Mratibu Elimu kata ya Kyela wilayani Kyela mkoani Mbeya Ester Richard akichangia mjadala wa Elimu katika Kongamano la Sekta ya Elimu lililofanyika mjini Kyela. 

BODI na Kamati za Shule mkoani Mbeya zimeagizwa kutekeleza majukumu zilizopewa ikiwemo kuwawajibisha wanafunzi wanaokwenda kinyume na sharia,kanuni na tararibu za shule ili kurejesha nidhamu mashuleni.

Agizo hilo lilitolewa na mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla kwenye Kongamano la Elimu wilayani Kyela ambapo amebainisha kuwa utovu wa nidhamu mashuleni ni moja kati ya changamoto zinazokwamisha maendeleo ya kitaaluma.

Makalla amesema jambo la kusikitisha ni kuwa wanafunzi wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya Utovu wa nidhamu mashuleni huku wajumbe wa Bodi na kamati za shule husika wakishuhudia kwa macho yao lakini hakuna hatua stahiki wanazochukua kama vyombo vilivyopewa wajimu wa kusimamia taasisi hizo.

Mkuu huyo wa mkoa pia ameonesha kusikitishwa na tabia za baadhi ya wazazi wanaokuwa na upendo uliopitiliza kwa watoto wao kiasi cha kuingilia utendaji wa walimu shuleni pale wanapowawajibisha wanafunzi.

Amesema wapo wazazi ambao malezi yao yamesababisha watoto kuwa legelege kwa kulelewa kama mayai na kuwasababishia walimu kukosa sauti juu ya watoto husika kwani pale wanapokosea na kuwajibishwa mashuleni wazazi huja juu na kwenda kuwakalipia walimu.

Aidha Makalla amesema ipo haja ya kurejeshwa kwa mfumo wa elimu ya kujitegemea ili kuwajengea wanafunzi mfumo wa kupenda shughuli mbalimbali za kujiingizia vipato wakiwa bado shuleni na kubainisha yuko yupo tayari kuwajibika iwapo itaonekana alikosea kurejesha mfumo huo.

No comments:

Post a Comment