Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, August 10, 2015

MATUKIO NANENANE MBEYA KATIKA PICHA



Waziri mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Meneja mashamba wa kampuni inayojishughulisha na masuala ya kilimo ya Buyuni Redd Farms(T) Ltd Segundwa Lesilwa katika banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya nanenane kanda ya nyanda za juu kusini.Kulia kwa waziri mkuu ni Naibu waziri wa Kilimo,chakula na Ushirika Godfray Zambi na mke wa waziri mkuu Mama Tunu Pinda.

Waziri mkuu Mizengo Pinda na mkewe mama Tunu Pinda wakiangalia mchele uliosindikwa na kufungwa katika vifungashio vya kisasa kazi inayofanywa na kampuni ya Mtenda Kyela Rice Supply ya mkoani Mbeya
 Mmoja wa wajasiriamali mkoani Mbeya Allan Mwaigaga ambaye sasa ni wakala wa usambazaji wa Trekta zinazozalishwa na kampuni ya Toyota akizungumza na wadau wa kilimo waliotembelea banda lake kwenye maonesho ya wakulima ya nanenane kanda ya nyanda za juu kusini akihamasisha vijana kuwekeza katika kilimo badala ya kupenda maisha ya kifahari kwa kununua magari ya gharama.




 Waziri mkuu Mizengo Pinda na viongozi wengine wakimwangalia mbwa aliyefundishwa kufanya shughuli mbalimbali kama binadamu ikiwemo kubeba mizigo.Mbwa huyo alikuwa kivutio kikubwa katika maonesha ya wakulima Nanenane kanda ya nyanda za juu kusini yaliyofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.






Mbwa aliyefundishwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kubeba mizigo akiwa amebeba begi dogo ndani ya viwanja vya maonesho ya Nanenane vya John Mwakangale


Kijana ambaye hakufahamika jina wala makazi yake mara moja akiwa mikononi mwa vijana wa Skauti wakimpeleka kituo kidogo cha polisi cha nanenane baada ya kumuokoa mikononi mwa wananchi waliokuwa wakimpiga wakimtuhumu kuiba simu ya kiganjani siku ya kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Nanenane kanda ya nyanda za juu kusini. 




No comments:

Post a Comment