Waziri wa nchi ofisi ya
rais Prof Mark Mwandosya akizungumza na wakazi wa mkoani Mbeya kwenye viunga
vya ukumbi wa Benjamini Mkapa jijini Mbeya jana alipotangaza nia ya kugombea
urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Viongozi wa jadi wakifuatilia kwa karibu sherehe za kutangaza nia..
WAZIRI
wa Nchi ofisi ya Rais Prof Mark Mwandosya leo ametanga nia ya kuwania nafasi ya
urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) huku akisema yeye si bingwa wa kujisifia
kama wanavyofanya wengine.
Prof
Mwandosya ambaye alivitumia viwanja vya Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo
Sokomatola jijini Mbeya,viwanja ambavyo ndivyo vilitumika kwenyemikutano ya
Mwalimu Julias Nyerere alipokuwa akihamasisha harakati za kutaka uhuru wa
Tanganyika alisema hana alichofanya yeye kama yeye bali yapo mengi aliyoyafanya
kwa kushirikiana na wadau wengine.
Akizungumzia
vipaumbele vyake,Prof Mwandosya alisema katika elimu angependa kuona elimu ya
msingi inakuwa ya kuanzia darasa la kwanza hadi kiidato cha nne huku pia
akisisitiza umuhimu wa jamii ya wanawake kupewa kipaumbele katika kupewa elimu.
Kwa
upande wa Sekta ya afya alisema kwa muda mrefu taifa limejikita katika kutenga
bajeti kubwa kwaajili ya matibabu badala ya kuwekeza kwenye mikakati ya kinga
jambo ambalo litawezesha serikali kuepukana na gharama kubwa.
Alisema
ni wakati kwa serikali kuhakikisha kila mdau wa sekta ya afya anawajibika ipasavyo
kwa kuiwezeshya jamii kujikinga na maradhi badala ya kuhangaikia matokeo ya
maradhi.
Akizungumzia
suala la amani na utulivu alisema ni jambo la msingi kwa jamii kuendelea
kutambua kuwa Amani na utulivu uliopo nchini ni tunu pekee kutoka kwa Mwenyezi
Mnungu hivyo walinzi wa kweli wanapaswa kuwa wao japo kuna haja pia ya
kuendelea kuimarisha vikosi vya ulinzi na usalama.
„Kwa
upande wa ajira kwa vijana,bado tuna changamoto,lakini hii ni kutokana na
vijana wengi kuwa na mawazo ya kuajiriwa zaidi kuliko kujiajiri.Tunapaswa
kufikiri zaidi na kuondokana na dhana ya kuuza vyetu badala ya mawazo na
dehamira mpya.Ni muhimu tukahamasioka hata kuvuka mipaka ya nchi yetu.hii
itatuwezesha kupata fedha nyingi kwa kuwa na watanzania wanaofanya shughuli zao
nje ya nchi”.
Waziri
huyo pia aliwatupia lawama baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakienda nje ya
nchi na kwenda kutoa matamko yenye kuisema vibaya nchi yao hatua aliyosema ni
ya kusononesha na haitofautiani na watanzania wengine ambao uzalendo kwa nchi
yao umepungua katika kuipenda nchi yao,kutothamini vitu vinavyozalishwa nchini
sambamba na kutoipenda lugha yao ya taifa yaani Kiswahili.
Katika
hafla hiyo ya kutangaza nia,wakazi mkoani hapa walimchangia Prof Mwandosya
zaidi ya shilingi milioni 10.7 kwaajili ya kuchukulia fomu ya kugombea urais
ambapo waziri huyo alisema atachukua fomu hiyo jumatano hii mjini Dodoma.
Awali
mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya siasa mkoani Mbeya Godfray Mwandulusya
alisema vyama vya upinzani mkoani hapa viko pamoja na Prof Mwandosya kutokana
na historia yake isiyomuonesha kuwa mtu mwenye kashfa katika nafasi alizowahi
kuzitumikia.
Kwa
upande wake mwakilishi wa viongozi wa kimila mkoani hapa Chifu Soja Masoko
alisema kiongozi anayehitajika wakati huu ni yule asiye na nia ya kuwagawa
watanzania badala ya kuwaunganisha.
No comments:
Post a Comment