January Makamba
akiwapungia mkono wananchi na wanachama wa CCM mkoa wa Mbeya wakati akishuka
kutoka garini, wananchi hao walifika hapo katika ofisi za CCM wila ya Mbeya
Mjini kwa aijili ya kumdhamini.
Katibu wa CCM
wliaya ya Mbeya Mjini, Kurwa Milonge akimkabidhi January Makamba fomu yenye
majina na sahihi za wanachama wa CCM waliomdhamini
January Makamba
akihutubia wanachi na wanachama wa CCM mkoani Mbeya mara baada ya kukabidhiwa
fomu yenye majina na sahihi za wanachama waliomdhamini
January Makamba akiweka sahihi katika kitabu cha wageni katika ofisi ya katibu wa CCM wilaya ya Mbeya Mjini mara baada ya kuwasili katika ofisihizo, kushoto ni mkewe Ramona Makamba
January Makamba
na mkewe, Ramona Makamba wakiwapungia mikono wananchi na wanachama wa CCM mkoa
wa Mbeya walipowasili katika viwanja vya ofisi za CCM wila ya Mbeya Mjini
HABARI KAMILI
NAIBU waziri wa
Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia January Makamba amepata wadhamini 1678 katika
viunga vya ofisi ya CCM mkoa wa Mbeya leo.
Akiwa mkoani Mbeya Makamba
licha ya kuponda makada wengine ndani ya chama hicho akiwalaumu kuwa wanatumia
fursa ya kuwapaka matope makada wengine waliotangaza nia na kuchukua fomu yeye
amesema mfumo wa mbio za kijiti ni aliyechoka kukimbiza kumpa aliye na nguvu
ili akimbize zaidi.
Amesema hatarajii kuona
CCM inatoa kijiti kutoka kwa mtu aliyechoka na kumpa mkimbizaji aliyechoka bali
itampa kijiti hicho mkimbiaji mpya na mwenye nguvu za kutosha kumudu kasi ya
mashindano ili kufikia malengo ya ushindi.
Amesema kwa sasa CCM
inapaswa kutambua kuwa wakati uliopo ni wa kukabidhi madaraka kwa uongozi wa
kisasa unaoendana na mambo ya kisasa yaliyopo badala ya kuendelea kuuacha kwa
kizazi kisichoendana na kasi iliyopo hali inayoweza kuzorotesha ustawi wa
kizazi chote.
No comments:
Post a Comment