Meneja wa Afya wa
Unicef kutoka Dar es salaam Dkt.Tadashi Yasuda akielezea Visababishi vya vifo vya wajawazito na watoto wachanga alipowasilisha mada ya mradi kwa mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro na wageni wengine.
Mwakilishi wa
shirika la KOICA nchini Seung Kim akibainisha namna shirika hilo lililodhamiria kusaidia katika kutekeleza mpango huu na namna fedha zilivyopatikana
Wajumbe wakiwemo wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa halmashauri na wanakamati za afya za wilaya wakifuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas
Kandoro akihutubia wajumbe waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mpango huu
Diwani wa kata ya Isanga jijini Mbeya Shekhe Dull Mohamed akitoa neno la shukrani.Ni baada ya mkuu wa mkoa kuzindua.
HABARI KAMILI
SHIRIKA la kusaidia
watoto Duniani(Unicef) limetaja mambo matatu makuu yanasosababisha vifo vya
wanawake wajawazino na watoto wachanga nchini na kubainisha kuwa iwapo jitihada
za dhati hazitafanyika kukabiliana na mambo hayo harakati za kupunguza vifo
hivyo haziwezi kuzaa matunda.
Meneja wa Afya wa
Unicef kutoka Dar es salaam Dkt.Tadashi Yasuda ameyataja mambo hayo kuwa ni
Kuchelewa kuchukuliwa kwa maamuzi ya mama mjamzito kwenye vituo vya huduma za
afya,Ukosefu wa miundombinu ya uhakika ya usafiri na pia Hali ya utoaji huduma
isiyoridhisha.
Katika hafla fupi ya
uzinduzi wa mpango wa miaka minne wa Kusaidia maisha ya Akina mama na Watoto
kwa halmashauri 10 za mkoani hapa unaofadhiliwa na shirika la Korea International
Cooperation Agency(KOICA) kupitia Unicef Meneja huyo amesema changamoto hizo ni
chanzo kikubwa cha vifo nchini.
Amesema katika kaya
nyingi nchini maamuzi ya kumpeleka wanafamilia kwenye vituo vya tiba
hutegemeana na wanaume jambo ambalo husababisha wajawazito wengi kuchelewa
kufikishwa kwenye maeneo hayo na kupewa huduma stahili.
Amesema pia changamoto
ya Usafiri inayotokana na ama uhaba wa vyombo vya usafiri au ubovu wa
miundombinu imekuwa ikikwamisha wajawazito na watoto wachanga kufikishwa kwa
wakati kwenye vituo vya tiba na wanapofikishwa tayari wanakuwa katika hali
mbaya.
Meneja huo amesema hali
ya utoaji huduma isiyoridhisha kwenye vituo vya tiba ni changamoto nyingine
ambayo hutokana ama na watoa huduma kutoijali kazi yao au uhaba wa rasilimali
watu na vitendea kazi.
Kwa upande wake mkurugenzi
wa Afya na Lishe wa Unicef Dkt.Sudha Shema ameshauri halmashauri zilizofikiwa
na msaada wa mpango huo kuweka mikakati ya dhati yenye kuwezesha kupunguza
changamoto kwenye sekta za afya ili kuendana na malengo ya milenia.
Akizungumzia mpango
huo,mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ametaka wadau wa sekta ya afya mkoani
hapa kutowaachia watu wachache kutekeleza mradi husika badala yake kila mmoja
awajibike kwa nafasi yake.
No comments:
Post a Comment