Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, June 4, 2015

NANE WAPANDISHWA KIZIMBANI KATAVI KWA KUMKATA ALBINO MKONO



WATU  wanane wamefikishwa  na kupandishwa kizimbani  katika Mahakama  ya Wilaya ya Mpanda  Mkoa wa Katavi   kujibu shitaka  la kumjeruhi kwa mapanga  na kisha kumkata  mkono  na kutomomea nao wa   mwanamke  mmoja  aitwaye Remi  Luchumi (30) mkazi wa Mwamachoma   Tarafa ya Mamba Wilaya ya Mlele na kisha kutokomea nao.

Watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani hapo jana  mbele ya Hakimu mkazi wa Mahakama  ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi  Odira   Amworo.

 Washitakiwa hao nane waliopandishwa kizimbani  ni  Alex Manyanza (24)  Nogele Maliganya (Hombohombo)  40   Galula  Nkuba(45)  Shile Jilala(27)  Masunga  Kashinje(34)  Maiku  Punga (27) Koga  Silanga(32) wote wakazi wa Kijiji cha Maji moto Tarafa ya Mamba Wilaya ya Mlele na  Salumu sawa Mkazi wa  Meatu Shinyanga.

Mwendesha mashita mwanasheria wa Serikali wa Mkoa wa Katavi  Hongera Mwakifimbo  alidai mahakamani hapo kuwa,  watuhumiwa  walitenda kosa  hilo  hapo Mei 14 mwaka huu   nyakati za  saa sita usiku nyumbani kwa wazazi wake na Albino huyo  katika Kijiji cha Mwamachoma.

Watuhumiwa wanadaiwa kwamba siku hiyo ya tukio  walikwenda nyumbani kwao na  Remi  Luchoma  na walimkuta akiwa amelala na kisha walimjeruhi kwa mapanga sehemu ya mkono wake na kisha walifanikiwa kumkata kingaja  cha mkono wake na kisha walitokomea nacho
  Baada ya kusomewa mashita na mwanasheria wa serikali   Mawiti Malifimbo  katika kesi hiyo ambayo ilimevutia hisia za watu wengi wa Mkoa wa Katavi.

Washitakiwa  wote kwa pamoja   walikana   kutenda kosa hilo  na   waliomba Mahakama iwape  dhamana kwa kuwa walikuwa na watu wa kuwadhani.

 Hata hivyo  maombi hayo yalipigwa vikali kwa kile kilichodaiwa na mwanasheria wa Serikali kuwa endapo washitakiwa watapewa dhamana wanaweza kuharibu ushahidi kwani  bado kuna watuhumiwa wengine  wanaendelea kutafutwa.

 Hakimu  Odira  baada ya kusikiliza maombi ya pande hizo mbili aliamuru washitakiwa  wapelekwe rumande hadi hapo Julai 15  ambapo kesi hiyo itakapo tajwa tena.

Tukio la kukatwa kwa mkono kwa Albino huyo limekuwa ni la kwanza  kutokea katika Mkoa wa Katavi tangia  kuanza kutokea  kwa mauaji ya Albino hapa nchini

KWA HISANI YA BLOGU YA PEMBEZONI KABISA.

No comments:

Post a Comment