Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, June 3, 2015

NDOMBOLO YA SOLO ATANGAZA KUMVUA UBUNGE MWANJALE




MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Anderson Kabenga ametangaza kuwania nafasi ya ubunge Mbeya vijijini kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwenye uchaguzi ujao.

Kabenga maarufu kama Ndombolo ya Solo ametangaza nia ya kuwania nafasi hiyo alipozungumza na Lyamba Lya Mfipa jijini Mbeya ambapo ameweka wazi kuwa kipindi alichokaa katika madaraka ya udiwani kwa miaka kumi ikiwemo mitano aliyoshika uenyekiti wa halmashauri kinatosha na sasa anataka ubunge.

Hata hivyo Kabenga hakuweka bayana kuwa kunuia kwake kuukwaa ubunge kunatokana na mbunge wa Sasa Luckson Mwanjale kushindwa kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo,badala yake alisema yapo mambo anayoona hayaendi sawa na kwa nafasi ya uenyekiti anashindwa kuyafanyia kazi.

Mwenyekiti huyo amesema miongoni mwa mambo yanayomsukuma kuwania nafasi hiyo ni kuvalia njua jukumu la kuipigia debe bajeti inayopitishwa na halmashauri atakapokuwa bungeni akisema kwa sasa kuna kusuasua katika kuipitisha bajeti inapofika kwenye ngazi ya bunge.

Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wake kwenye halmashauri,amesema kupatikana kwa hati safi kutoka kwa mkaguzi na msimamizi wa hesabu za serikali(CAG) ni sehemu ya mafanikio ya kujivunia.

Kabenga pia amewataka wananchi kuwapuuza watu wachache aliosema wanajariobu kumchafua kwa kumtaja kuwa mmoja wa wafuasi wa wagombea wa nafasi ya urais wanaotumia fedha nyingi kuwarubuni wananchi akisema malengo yake ni kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na si kusaka utajiri.

No comments:

Post a Comment