Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, May 26, 2012

YATIMA 140 KUPEWA KITUO


WATOTO zaidi ya 140 walio yatima na wanaoishi katika mazingira magumu katika jijiji cha Mahango wilayani Mbarali wanatarajiwa kunufaika kwa kupata malezi baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo kinachojengwa kijijini hapo.

Ujenzi wa kituo hicho unaofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali na lisilo na maslai yoyote la  “BEZMANY” la  nchini Czech Republic utagharimu zaidi ya shilingi milioni 170.

Akizungumza na Lyamba Lya Mfipa,mwakilishi wa Bezmany katika nchi zilizopo barani Afrika Chriss Zacharia, alisema lengo la kujenga kituo hicho ni kuwasaidia watoto wa aina hiyo aliosema takwimu zinaonesha uwepo wao kwa wingi kijijini hapo.

Alisema tayari fedha hizo zimeanza kutumika kwa ujenzi wa bweni la wavulana ambalo mpaka sasa limegharimu shilingi milioni 90.

Alifafanua kuwa mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa bweni hilo utafuata ujenzi wa sehemu ya chakula,jiko na stoo  utakao gharimu milioni 29 na pia bweni la wasichana litakalogharimu shilingi milioni 55.

 “Kwa ujumla tunataraji kuwa na mabweni mawili kwaajili ya wavulana na wasichana.Kila bweni litakuwa na uwezo wa kuchukua watoto 70 kwa wakati mmoja” alisema Zacharia.

Zacharia alisema shirika halitoishia katika ujenzi pekee bali lipo tayari kugharamia chakula,mavazi na malazi kwa watoto wote watakaoishi kituoni hapo.

Alizitaja huduma nyingine zitakazogharimiwa na shirika kuwa ni  pamoja na kutoa elimu bora,afya na kuwaandaa watoto kuingia kwenye jamii kwa maisha yao ya baadae.

Alisema tayari shirika hilo likishirikiana  na ubalozi wa Marekani limeweza kufungua shule ya awali ya Kajunjumele Nursery School kwa ajili ya watoto yatima wenye umri  kuanzia miaka3-6 wanao jifunza kusoma,kuandika na somo la hisabati.

Alisema,  katika mradi wa kusaidia shule shirika limeweza kununua madawati kwa shule za Mahango na Simike jijini Mbeya na,kufanya  ukarabati  wa madarasa katika shule za msingi kama vile kisa wilayani Rungwe,Galula wilayani Chunya na Ilasilo Mbeya Vijijini

No comments:

Post a Comment