Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, May 2, 2012

SILINDE MBUNGE HALALI MBOZI MAGHARIBI

MAHAKAMA Kuu ya Rufaa Kanda ya  Mbeya imeondoa shauri la kesi ya rufaa iliyopelekwa na Dkt.Lucas Siame(CCM) kupinga hukumu iliyotolewa Julai mosi, mwaka jana dhidi ya ushindi wa Mbunge wa Jimbo la Mbozi Magharibi David Silinde(CHADEMA) hivyo kumfanya Silinde kuwa mbunge halali wa jimbo hilo.
 Mamuzi huo ulitolewa leo  na Majaji watatu waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo chini ya Mwenyekiti wao  Jaji Januari Msofee ambao ni Jaji William Mandia na Jaji Mbarouk S.Mbarouk baada ya Wakili wa mlalamikaji Victor Mkumbe kuwakilisha ombi la kutaka kuondoa shauri hilo mahakamani hapo.
Akiwasilisha ombi hilo mbele ya mahakama hiyo ya rufaa wakili Mkumbe amesema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya mlalamikaji kuonyesha nia ya kutotaka kuendelea na kesi hiyo
Baada ya maelezo hayo jaji Msofee amemhoji wakili wa mlalamikiwa Benjamini Mwakagamba kama angekuwa na la kusema baada ya kusikia ombi la mlalamikaji naye akakubaliana na ombi hilo lakini akiitaka mahakama kumwamuru mlalamikaji kumlipa gharama alizotumia.
 Akisoma hukumu hiyo Jaji Mandia amrsema kuwa mahakama ya rufaa imekubali ombi hilo na hivyo shauri hilo limeondolewa kwa mujibu wa kanuni ya 4(2)(a).

No comments:

Post a Comment