Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, May 9, 2012

WAHABESHI 6 WAFA BAADA YA FUSO KUTUMBUKIA MTONI

WAHAMIAJI haramu sita raia wa Ethiopia wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kutumbukia mtoni.

Msemaji wa jeshi la polisi mkoani Mbeya Mbogela Majaliwa amesema ajali hiyo imetokea Mei 7 mwaka huu majira ya saa 4:30 usiku katika mto Lutete uliopo kijijini Luswiswi tarafa ya Bundali wilayani Ileje.

Majaliwa amesema wahabeshi hao wakiwa jumla 67 wote wanaume walikuwa wakitokea Tanga na lengo likiwa ni kwenda Afrika kusini kupitia nchi jirani ya Malawi kwa kutumia gari lenye namba T 934 AAR Mitsubish Fuso mali ya Mandali Msuya.

Amewataja waliofariki dunia na kutambuliwa kuwa ni Lamasa Lamole na wawili walio tambuliwa kwa jina moja moja ambao ni Tamlat na Ibrahim na wengine watatu bado hawajatambuliwa na miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Ileje.

Kwa upande wa majeruhi,kumi wamelazwa katika hospitali ya misheni Isoko na watatu kwenye hospitali ya wilaya huku wengine 48 walionusurika wakiendelea kushikiliwa katika kituo cha polisi cha wilaya ya Ileje na Dereva ambaye bado hajafahamika alikimbia baada ya tukio.

No comments:

Post a Comment