MWITO
umetolewa kwa wakazi wilayani hapa kuhakikisha wanatambua kuwa uwajibikaji
unaopaswa kuhojiwa si kwa upande wa viongozi pekee bali pande zote ikiwamo wao.
Hayo
yameelezwa na katibu tawala wa wilaya hiyo Josephat Kakuru alipokuwa akifungua
mdahalo wenye lengo la kuimarisha uwazi,uwajibikaji na uhusiano baina ya
viongozi waliochaguliwa na wananchi uliaondaliwa na mtandao wa asasi zisizo za
kiserikali wilayani Nkasi(NKANGONET)na kufanyika katika kata ya Kirando.
Kakuru
amesema watu wengi wamekuwa wakihoji juu ya uwajibikaji wa viongozi pekee na
kutoa malalamiko mengi wakiwalenga viongozi wanaoonekana kutowajibika ipasavyo
wakisema wanakwamisha maendeleo yao.
Kwa
upande wake mbunge wa Nkasi kaskazini Ally Kessy alikiri kuwepo kwa watu wengi wanaopenda
kuhoji utekelezaji wa majukumu ya viongozi wao lakini wao hujitoa ni kama si
sehemu ya kumsaidia kiongozi akatimiza wajibu wake.
Kessy
ametolea mfano kwa vitendo vya wizi wa fedha za serikali vinavyofanywa na
baadhi ya maafisa wa mamlaka ya mapato TRA na mabwana samaki katika mwambao wa
ziwa Tanganyika akisema licha ya wananchi kushuhudia uozo unaofanywa bado
hawatoi taarifa mahali popote.
No comments:
Post a Comment