TIMU shiriki za mashindano ya michezo mbalimbali kwa
shule za Sekondari (UMISETA) mkoani hapa jumatano hii jioni zitaingia kambini
tayari kwa mashindano hayo yatakayoanza kimkoa Mei 31 mwaka huu.
Afisa michezo mkoa wa Mbeya George Mbijima ameiambia LYAMBA LYA MFIPA kuwa mashindano hayo yataendeshwa kwa muda wa siku nne katika viwanja vya
shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya na yatashirikisha timu kutoka
halmashauri nane zilizopo mkoani hapa.
Mbijima amesema mashindano hayo pia yatalenga
kuchagua wachezaji wa timu itakayouwakilisha mkoa katika mashindano ya Umiseta
kanda ya nyanda za juu kusini yatakayofanyika mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
Ameitaja baadhi ya michezo katika mashindano kuwa ni
mpira wa miguu na mkono,wavu,riadha,kikapu,mpira wa meza ma bao yote hiyo ikiwa
ni kwa wavulana na wasichana pamoja na mchezo wa netibal kwa wasichana pekee.
Afisa michezo huyo amesisitiza kuwa wachezaji wa
timu shiriki ni lazima wawe wanafunzi katika shule za sekondari walio katika
utaratibu maalumu unatambuliwa na serikali na si mamluki kutoka mitaani,vituo
vya elimu binafsi wala wanaojiandaa kurudia mitihani ya kitaifa ya kidato cha
nne au cha sita.
Aidha,ametoa wito kwa wazazi na walimu kuwaruhusu
watoto ama wanafunzi wao kushiriki mashindano hayo kwakuwa hiyo pia ni fursa ya
wao kuonesha vipaji walivyonavyo na pia kwa kuzingatia umuhimu wa michezo
katika afya za miili yao.
No comments:
Post a Comment