Chifu
Kiongozi wa Kabila la Kisafwa Bwana Roketi Mwanshinga(Kulia) akiongoza
jopo la Machifu kuweka tambiko la kukemea vitendo vinavyohusisha na
Imani za kishirikiana katika Shule tatu za Msingi katika Kata ya Itenzi.
Chifu
Kiongozi wa Kabila la Kisafwa Bwana Roketi Mwanshinga(pichani kushoto )
akiongoza jopo la Machifu kuweka tambiko la kukemea vitendo
vinavyohusisha na Imani za kishirikiana katika Shule tatu za Msingi
katika Kata ya Itenzi na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Tambukareli
(pichani kulia) .
Machifu
wakiingia katika Ofisi ya Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi ya
Tambukarelikufanya tambiko la kukemea vitendo viovu vinavohusishwa na
Imani za kishirikina katika Shule tatu za Msingi, zilizopo Kata ya
Itenzi.
Machifu
wakiingia katika madarasa na kufanya tambiko la kukemea vitendo viovu
vinavohusishwa na Imani za kishirikina katika Shule tatu za Msingi,
zilizopo Kata ya Itenzi.
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi Igombe wakiwasikiliza Machifu licha ya mvua kubwa
iliyokua ikiendelea kunyesha, katika zoezi la tambiko la kukemea vitendo
viovu vinavyohusishwa na Imani za kishirikina.
Wananchi
waliojitokeza kutoka Kata ya Itenzi katika zoezi la Machifu waliofika
katani hapo kutambika kwa lengo la kukemea vitendo viovu
vinavyohusishwa na Imani za kishirikina.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Machifu
wa kabila la Kisafwa Mkoani Mbeya waliamuru kusitishwa kwa masomo kwa
siku moja katika Kata ya Itenzi Jijini Mbeya, kutokana na wanafunzi wa
jinsia ya kike kuanguka, kupoteza fahamu na kuwanyong’oshesha nguvu.
Tukio
hilo limehusisha Shule za msingi za Gombe, Tambukareli na Mwasote,
zoezi lililofanya na Chifu kiongozi wa kabila hilo Roketi Mwanshinga,
akisaidiana na zaidi ya mchifu 30.
Pia
zoezi hilo limehudhuriwa na Diwani wa Kata ya Itenzi Mheshimiwa Frank
Mayemba na Askari wa Jeshi la Polisi na Ulinzi shirikishi L.M Kiyeyeu Mei 2 mwaka huu.
Kabla
ya kuanza kazi hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wananchi wanaozizunguka
shule hizo, Chifu Mwanshinga alishusha lawama kwa Wachungaji wa
madhehebu na makanisa mbalimbali Mkoani hapa, kutokana na kupokea
waumini kwa kivuli cha kuokoka bila kuwauliza machifu.
Amesema
kwani wao wanafahamu hawajaacha tabia zao za awali ndio maana vitendo
hivi vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku huku makanisa hayo yakichipuka
kama uyoga.
Chifu
Mwanshinga ameenda mbali zaidi kwa kusema daima maisha yao ni duni,
hivyo hufanya vitendo hivyo kwa nia ya kujipatia pesa wanajidanganya
kwani pesa hupatikana kwa kufanya kazi kwa bidii na si vinginevyo.
Mkusanyiko
huo umefanyika baada ya watoto wanaosoma katika shule hiyo hususani
wasichana darasa la tano ndio wanaoathirika zaidi na ugonjwa wa kuanguka
na kupoteza fahamu na kuwanyong’onyesha nguvu na hivyo kushindwa
kuendelea na masomo na kuwapeleka nyumbani kwao.
Katika
mkutanoi huo Machifu wameagiza yeyote anyejihusisha na masuala hayo
aache mara moja na kutoa onyo yeyote atakayekaidi agizo hilo atatembea
barabarani akiwa kichaa.
Aidha
katika hali ya kusafisha mazingira hayo machifu wote walipita katika
madarasa yote ya shule zote tatu na kwamba kuanzia sasa watapiga kambi
kwa muda wa juma moja hatimaye kukomesha kabisa vitendo hivyo ambavyo
huathiri huduma za maendeleo ya elimu na kiuchumi mkoani hapa.
Kutokana na kukerwa na suala hili machifu wameagiza wazazi wote wakeshe kwenye shule hizo ili kukomesha kabisa vitendo hivyo.
Kwa
upande wake pia Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Bwana Deusdedit Maseke
amewashukuru wazazi kwa kuitikia wito wa kufika shuleni hapo na kuonesha
jinsi walivyokerwa na jambo hilo.
Shule
kadhaa mkoani Mbeya zimekubwa na janga la ushirikina na kupelekea
kufungwa kutokana na vitendo vya kishirikina ikiwemo Shule ya Juhudi
iliyopo kata ya Iganzo ambapo Ofisi ya Mwalimu Mkuu alisilibwa kinyesi
pamoja na ofisi nyingine ya walimu mbali ya kusilibwa kinyesi vyombo vya
chakula vilitapakaa kinyesi.
No comments:
Post a Comment