Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro ametolea ufafanuzi suala la kujiuzuru kwa
aliye kuwa Mkuu wa wilaya ya Mbozi Ndugu
Gabriel Kimolo .
Akizungumza na waandishi wa habari ofisi
kwakwe Kandoro amesema hadi sasa Rais
Jakaya Kikwete hajateua wakuu wa wilaya nchini kwa sababu ambazo zipo ndani ya
uwezo wake mwenyewe na yeye hawezi kuzielewa.
Amesema
siyo kweli kuwa Kimolo amejiuzuru, kwani tayari alikuwa na taarifa kuwa hawezi
kuteuliwa kuendelea na wadhifa huo tangu Machi 23, mwaka huu, hivyo aache kutoa
visingizio visivyo na mashiko.
Ameongeza
mara kuwa baada ya kupewa taarifa za kutoteuliwa tena, Machi 24, mwaka huu
Kimolo alimfuata Mkuu wa mkoa ofisini kwake na kulalamika kuwa amefanya kazi
kwa uaminifu na uadirifu hivyo ameuamia kwa kupewa taarifa za kutoteuliwa tena.
Kwa mujibu
wa Kandoro, barua hiyo ya Kimolo ambayo ameipata leo (jana), asubuhi
ataifikisha kwenye mamlaka ya utumishi, lakini akamshauri Kimolo ni heri
angeondoka kwa amani na siyo kuanza kutoa visingizio visivyo na msingi.
Mkuu wa
mkoa amesema, ameona ni vyema aliweke wazi jambo hilo kwa vyombo vya habari ili
yeyote anayetaka kujiuzuru basi afanye hivyo kwa nia njema na siyo kuwachafua
wengine.
Wakati huo
huo, Kandoro ameweka wazi nia yake ya kumfikisha mwandishi wa habari wa
Tanzania Daima, aliyeandika katika gazeti hilo la Machi 5, mwaka huu kuwa
Kimolo amesema amefikia adhma hiyo kwa kukosa ushirikiano na Wizara ya Kilimo
pamoja na yeye.
Ameeleza
kuwa waandishi wa habari ni mashahidi wa
mgogoro uliopo wilayani Mbozi, kuhusu upigwaji marufuku ununuzi wa Kahawa
mbichi (Red Cherry), hivyo hiyo haiwezi kuwa sababu ya Kimolo kumchefua yeye
gazetini.
Amesema kwa
kuwa hilo halikuelezwa na Kimolo, bali mwandishi huyo wa Tanzania Daima,
ameamua kuliweka na kumchafua basi atafuata taratibu kwa kukutana na Kamati ya
Maadili ya Chama Cha Waandishi wa Habari Mbeya, ili kuliweka sawa.
Ameongeza
iwapo hatatendewa haki basi atafuata utaratibu mwingine kwa kulifikisha hilo
mbele ya Baraza la Habari Tanzania , kwa hatua zaidi ili aweze kutendewa haki
kwa kuchafuliwa mbele ya umma.
Kimolo
ametangaza uamuzi huo (Mei 4) katika
kikao chake na waandishi wa habari kilichofanyika katika hoteli ya Beaco
iliyopo Forest mpya jijini Mbeya.
No comments:
Post a Comment