Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, May 28, 2012

WAJAWAZITO WAJIFUNGULIA GIZANI


WANAWAKE wajawazito wanaopata huduma zao katika kituo cha afya cha Kirando wilayani hapa wanalazimika kujifungulia gizani kufuatia uhaba wa mafuta kwaajili ya jenereta unaokikabili kituo hicho.Mwandishi mkuu wa Lyamba Lya Mfipa Joachim Nyambo akizungumza na mama aliyekutwa anamlea mgonjwa ambaye ni mtoto wake katika wodi ya watoto kwenye kituo cha afya cha Kirando Uchunguzi uliofanywa na Lyamba Lya Mfipa na kuthibitishwa na uongozi wa kituo hicho umebaini wajawazito wanaotoka katika familia masikini kuwa na wakati mgumu mno wanapokwenda kujifungua kituoni hapo.

Hali hiyo inatokana na kila mjamzito ama mgonjwa yeyote anayelazwa katika kituo hicho ambacho wakazi wa vijiji vilivyopo pembezoni na ndani ya ziwa Tanganyika wanakiona kama hospitali ndogo kutakiwa kwenda na vibatali,karabai ama taa ya mafuta kutoka majumbani mwao.


Iwapo mgonjwa aliyelazwa kituoni hapo atakosa uwezo kabisa wa kuja na kibatari,karabai ama taa basi hulazimika kukaa gizani usiku kucha iwapo katika wodi alimolazwa hakutakuwa na mgonjwa mwingine anayetoka kwenye familia iliyo na unafuu wa kiuchumi.Victoria Mafulwa(Wa kwanza kulia) mwanamke aliyelazimika kufanyiwa upasuaji baada ya mimba yake kuharibika kutokana na kuchelewa kufikishwa katika kituo cha afya akitumia usafiri wa boti ya kukodi akizungumza na Lyamba Lya Mfipa 
 
Uchunguzi wa kina wa Lyamba Lya Mfipa pia umebaini hali kuwa mbaya kwa wagonjwa hususani wajawazito wanaokwenda hapo na kutakiwa kufanyiwa upasuaji ambapo pia hutakiwa kununua mafuta ya jenereta ndipo wahudumiwe na iwapo watakosa basi huwa na wakati mgumu iwapo hawatojitokeza wasamalia wema kuwachangia.

KWA MWENDELEZO WA HABARI HII ENDELEA KUTEMBELEA Lyamba Lya Mfipa ..............

No comments:

Post a Comment