Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, May 16, 2012

WAKUU WA WILAYA WAAPISHWA

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro leo amewaapisha wakuu wapya wa wilaya nane zilizopo mkoani hapo.

Wakuu wa wilaya walio apishwa ni pamoja na mkuu wa wilaya ya Chunya anaeendelea kuiongoza wilaya hiyo kwa ,mara nyingine Deodatusi Kinawiro na mkuu wa wilaya mpya ya Momba Abihudi Saideya.

Wengine ni Maichael Kadege wa Mbozi,Chrispin Meela wa Rungwe,Gulamhussein Kifu wa Mbarali,Nonman Sigalla wa Mbeya,Margareth Malenga wa Kyela na Rosemary Senyamule wa Ileje.

Akizungumza baada ya kuapisha wakuu hao wa wilaya,mkuu wa mkoa Kandoro amewataka kufanya kazi kwa kufuata misingi ya uadirifu ili kulinda heshima yao,familia zao pamoja na Rais Jakaya Kikwete aliyewateu.

Naye mkuu wa wilaya ya Rungwe bwana Chrispin Meela ameahidi kufanya shughuli zake kwa kushirikiana kwa karibu na watendaji katika halmashauri na wananchi kwa ujumla ili kuleta ufanisi katika shughuli zake.

No comments:

Post a Comment