MBUNGE wa Nkasi Kusini Desderius Mipata amewataka akina mama kuzitambua haki zao ili kuleta ustawi katika jamii na kuondokana na hali ya kuonekana kama watumwa mbele za waume zao.
Mipata
alitoa changamoto hiyo alipokuwa akichangia moja ya mada katika mdahalo wa
kujadili masuala ya Jinsia,Haki za wanawake na watoto uliofanyika katika kata
ya Kipande ukiwa umeandaliwa mtandao wa asasi zisizo za kiserikali wilayani
Nkasi(NKANGONET) na kudhaminiwa na shirika la The Foundation for Civil Society.
Mipata
alisema ni kutokana na wanawake wengi nchini kutozitambua haki zao wameendeleo
kuonekana kama vibarua hasa kwa waume zao mara tu wanapoolewa dhana aliyosema
imepitwa na wakati.
Alisema
ni wakati sasa kwa wanawaake kusimamia haki zao ili wawawezeshe pia waume zao
kuzitambua na kuzithamini haki hizo na hatimaye jamii itaishi kwa misingi ya
kutambua umuhimu wa kila jinsi kwa nyingine.
Mbunge
huyo alilalamikia pia unyanyasaji unaofanywa dhidi ya wazee akisema licha ya
kufanya kazi kubwa ya kuzitumikia familia na kulijenga taifa lao mpaka kufikia
umri wao bado hawathaminiwi kabisa.
Alisema
wazee wameendelea kunyimwa haki zao za msingi ikiwemo ya kuishi pasipo
kubughudhiwa badala yake kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili wanaitwa
wachawi eti tu kwakuwa wanamacho mekundu.
Alisema
pamoja na changamoto zote hizo bado pia wazee wanapewa mzigo wa kulea wajuu
waliozalishwa hovyo na watoto wao na kuwatelekeaza wakati ilipaswa uwe wakati
wao kulelewa na watoto hao.
Naye
mmoja wa wadau waliohudhuria mdahalo huo mzee John Kauzeni alilalamikia
serikali kwa kutotimiza ahadi ya kutoa matibabu bure kwa wazee akisema iliishia
kutoa vyeti vya uzee pekee lakini kila wanapokwenda kupata matibabu wamekuwa
wakiambiwa hakuna dawa.
“Wengi
tuliisifia sana serikali yetu baada ya kutoa vyeti vya kututambua wazee na
kuagiza yawepo madirisha maalumu kwaajili yetu.Lakini utekelezaji wa sera hii
hauonekani.Kila ukienda unaambiwa hakuna dawa na unatakiwa ukanunue katikaa
maduka ya watu binafsi” alisema.
Kwa
upande wa elimu kwa toto,ilijadiliwa upo utofauti mkubwa kati ya yule
aliyeishia kidato cha nne na hakufaulu ikilinganishwa na aliyeishia darasa la
saba.
No comments:
Post a Comment