Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, May 21, 2012

MWENGE WAMULIKA UFISADI MBARALI


MKIMBIZA mwenge mkuu kitaifa Olnest Mwanosa ameikataa taarifa ya ujenzi wa ofisi ya afisa tarafa ya Ilongo wilayani Mbarali kutokana na ujenzi huo kutoendana na kiasi cha fedha kilichotumika.

Mwanosa aliikataa taarifa hiyo mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika jingo hilo ambalo ujenzi wake ulianza Juni 2011 na mpaka sasa zaidi ya shilingi milioni 28 zimetumika.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo hilo kwa niaba ya afisa tarafa,afisa mtendaji wa kata ya Chimala alisema hadi kukamilika kwa ujenzi huo zaidi ya shilingi milioni 31 zitatumika.

Lakini Mwanosa alipinga matumizi hayo ya fedha akisema kiasi kilichotumika ni kikubwa ikilinganishwa na kazi inayoonekana kufanyika hivyo ipo haja ya wahusika wa ujenzi huo kutoa majibu yatakayoondoa hoja ya matumizi mabaya ya fedha zilizotengwa.

Alizitaja kasoro zinazoonekana katika jingo hilo pamoja na udogo wake ikilinganishwa na fedha zilizotengwa kuwa ni kuta kuanza kupasuka nyufa hata kabla ya ofisi kuanza kutumika,fremu za madirisha na milango kutokuwa na vigezo vinavyostahili kwa jingo kama hilo.

“Hata kwa hesabu ya kawaida mtu binafsi ukampa milioni 30 hawezi kujenga kajengo kama haka,lazima ataibuka na jingo kubwa,la kisasa na linalopendeza sasa mpaka leo zimetumika zaidi ya milioni 28 kwa jingo hili dogo namna hii.Hapa napata sababu ya kuwa na shaka kuwa huenda kuna mbinu chafu ya mtu kupitujenzi huu nay eye akawa anajenga kwake”

“Tumepita pale Vwawa wilayani Mbozi kule tulizindu jengo pia la afisa tarafa ambalo wametumia fedha kidogo sana mpaka kukamilisha pamoja na samani za ndani.Linapendeza na kweli ukiona unaridhika kuwa kazi imefanyika sasa iweje ninyi mtumie fedha zote hizo kwa jingo kama hili nab ado halijakamilika jamani” alihoji.

Aliuagiza uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo kujipanga upya kwa kuhakikisha mkandarasi aliyehusika na ujenzi wa jengo hilo anarudia kazi yake vinginevyo hatua zaidi za ufuatiliaji zitachukuliwa.

Aliwaasa viongozi kuwa makini katika ufuatiliaji wa maendeleo ya miradi mbalimbali kwenye maeneo yao badala ya kubaki ofisini na kusabaisha serikali iendelee kupakwa matope kutokana na miradi kutoendana na fedha zinazotumika.

No comments:

Post a Comment