Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, May 17, 2012

MAFISANGO KUAGWA KESHO

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgoWezTES4lR60ztBBC8vluI1hniN2co9qSe4JekbvaE39YqvOXc9rL7GomVR61OHa4UiDLe1JGa_z902ah2iquj0ElEJ8sam0ZRoB_FW6aFVbROIltfZ5epVpz_Nns83106yxTyTo_zbA/s1600/%253D%253Futf-8%253FB%253FbXV0ZXNhIG1hZmlzYW5vLmpwZw%253D%253D%253F%253D-742547
MPENDWA WETU MAFISANGO ATAAGWA KESHO SAA NNE ASUBUHI TCC CLUB CHANG'OMBE BADALA YA LEADERS CLUB

Mashabiki wa soka nchini Rwanda wanaomboleza kifo mchezaji soka wa kimataifa kutoka nchini humo Patrick Mafisango, mwenye umri wa miaka 32.
Mafisango, alikuwa amechaguliwa kuchezea kikosi cha kitakachowania kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 dhidi ya Algeria.
Alifariki katika ajali ya barabarani asubhi ya kuamkia leo mjini Dar es Salaam Tanzania.
Mchezaji huyo wa kiungo cha kati, anayechezea kilabu ya Simba nchini Tanzania, ndio alikuwa amerejea tu kutoka Sudan ambako timu yake ilishindwa katika michuano ya kuwania kombe la Confederation mwsihoni mwa wiki.
Kocha wa kilabu hiyo ameelezea kuhuzunishwa sana na tukio hilo.
Mafisango alifariki katika ajali iliyohusisha pikipiki na gari wakati gari alipokuwa anaenesha lilipoteza mwelekeo na kuanguka kwenye mtaro.
Alikuwa mchezaji mwenye mabao mengi msimu huu wa mechi za ligi ya Tanzania kwa kuingiza magoli, 12 na aliitwa na kocha Sredrojevic kushiriki mechi ya kufuzu kwa michauano ya kombe la dunia itakayofanyika mwezi ujao.
PICHA ZOTE NA HABARI KWA HISANI YA MITANDAO NA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI

No comments:

Post a Comment