Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, January 15, 2013

WAWILI WAZIKWA HAI

WATU wawili wakazi wa kijiji cha Ivuna wilayani Momba wamezikwa wakiwa hai baada ya wakazi wenzao kuwatuhumu kuwa ni wachawili. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwani Athumani alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea siku ya jumapili iliyopita ambapo aliwataja waliozikwa kuwa ni Mizinara Matela na Ernest Molela wote wakazi kijijini hapo. Kamanda Athumani alisema wakazi hao walikuwa wakituhumiwa na wanakijiji wenzao kuwa walihusika na kifo cha ndugu yao aliyemtaja kwa jina la Nongwa Molela aliyekufa baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Alisema baada ya maziko ya Nongwa ndipo wakazi wa kijiji wakiwemo ndugu wa marehemu walianza kuwanyooshea vidole watu hao wawili wakisema ndiyo waliomuu na kuchukua uamuzi wa kuanza kuwapiga. Alifafanua kuwa kabla ya kuwazika wakiwa hai kundi la wanandugu hao waliwapiga wawili hao kwa marungu na mawe na kabla ya kuwaua wakawatupia kwenye kaburi moja na kuwafukia humo. Baada ya kuwazika wakiwa hai,kundi la wanandugu hao lilikwenda nyumbani kwa Ernest na kuiteketeza nyumba yake kwa moto. Mpaka anazungumza na mwandishi wa habari hizi shughuli ya kufukua miili ya watu hao ilikuwa ikiendelea kwa lengo la kufanyiwa uchunguzi ambapo alifafanua kuwa baada ya uchunguzi huo kila mwili utazikwa kwenye kaburi lake. Aidha kamanda huyo alisema mpaka sasa watu wawili wanashikiliwa ambapo inasadikiwa kuwa ndiyo waliongoza kundi lililotenda ukatili huo lakini hakuwataja kutokana na sababu alizosema ni za kiusalama. Hii si mara ya Kwanza kwa matukio ya watu kuzikwa wakiwa hai kwa tuhuma za uchawi mkoani Mbeya kwani mwaka jana pia matukio hayo yalikuwa yakielewa kufanyika kwa usiri mkubwa lakini ilikuja kubainika siku ambayo Chifu Merere wa kabila la Wasangu aliponusurika kuzikwa akiwa hai na wakazi wa kijiji cha Ruiwa wilayani Mbarali.

No comments:

Post a Comment