Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, January 22, 2013

MUME AJINYONGA BAADA YA KUMNYONGA MKE

WATU wane wamefariki dunia mkoani Mbeya katika matukio matatu tofauti likiwemo la mume kujinyonga kwa kamba ya manira muda mfupi baada ya kumnyonga shingo hadi kumuua mkewe kutokana na wivu wa mapenzi. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwan Athuman aliwataja marehemu katika tukio hilo kuwa ni Richard Mwakalukwa(23) na mkewe Agnes Kalinga(18) wote wakazi katika kitongoji cha Mkeje kijiji cha Mwalisi kata ya Ngana wilayani Kyela. Kamanda Athuman alisema tukio hilo lilitokea Januari 21 mwaka huu majira ya saa 9:00 alasiri ambapo wakiwa chumbani kwao mume alimnyonga shingo mkewe mpaka kuivunja na baada ya kuona amemuua akachukua kamba ya manira na kujinyonga katika mti wa mkorosho nje ya nyumba yao. Alitaja chanzo cha mauaji hayo kuwa ni wivu wa mapenzi kwani mume Mwakalukwa kwa muda mrefu alikuwa akimtuhumu mkewe kutokuwa mwaminifu katika ndoa yao kutokana na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine. Katika tukio jingine lililotokea Januari 21 majira ya saa 12:30 jioni katika kijiji cha Hanseketwa wilayani Mbozi barabara ya Mbeya/Tunduma Gari lenye namba T 451 BRK Toyota Coasta lililokuwa likiendeshwa na Willy Songelamaarufu kama Muasisi(46) liligonga pikipiki yenye namba T 201 CCT aina ya T-Better na kusababisha kifo cha dereva wa pikipiki hiyo Tito Nyondo(20) mkazi wa Tunduma. Ajali hiyo pia alimsaababishia majeraha mwanafunzi wa shule ya sekondari Msika Baraka Nyondo(19) ambaye amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mbozi iliyopo katika mji mdogo wa Vwawa. Kamanda Athumani alisema tukio la tatu ni la kifo cha mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya Mwanyanje Halaika Bushiri(7) kilichosababishwa na ajali ya moto iliyotokea nyumbani kwao Uyole jijini Mbeya. Alisema tukio hilo lilitokea januari 21 majira ya 7:45 za mchana wakati mtoto huyo alikuwa amelala kwenye kochi lililokuwa kwenye korido ulipoanzia moto lakini baadaye ukazimwa.

No comments:

Post a Comment