Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, January 8, 2013

MBEYA TAYARI KWA LIGI MKOA

HATIMAYE cha soka mkoani Mbeya(MREFA) kimetangaza rasmi tarehe ya kuanza kwa michuano ya ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa ambapo sasa itaanza kutimua vumbi Januari 19 mwaka huu. Katibu wa Mrefa Seleman Haroub amesema kuwa kuchelewa kuanza kwa ligi hiyo iliyopaswa kuanaza Septemba mwaka jana kulitokana na uongozi mpya kukuta chama hakina fedha za kuendeshea ligi ulipoingia madarakani. Hata hivyo alisema kufuatia ukata unaokikabili chama pamoja na vilabu 17 vitakavyoshiriki uendeshaji wa ligi hautakuwa wa michezo ya nyumbani na ugenini kama shirikisho la soka nchini TFF lilivyoagiza badala yake itaendeshwa kwa mtindo wa ligi katika vituo. Alisema timu shiriki zimegawanywa katikaa makundi mawili ya A na B ambapo kundi A zipo timu za Airpot Rangers na Eleven Boys za Mbeya mjini,Kimondo Sc na Hollywood za wilayani Mbozi,Masukuru FC na Muungano FC za wilayani Rungwe,Boma FC ya Kyela na Chemchemu FC ya Chunya. Kwa upande wa kundi B zipo Juhudi FC na Wenda FC za Mbeya vijijini,Black Scopion na Magereza Ruanda za Mbeya mjini,Tukuyu Stars ya Rungwe,Mahongole FC ya Mbarali,Biashara FC ya Chunya na Ichenjezya Boys ya Mbozi. Alisema ligi hiyo itatanguliwa na mchezo wa ngao ya hisani kati ya Boma Fc ya Kyela na Eleven Boys ya Mbeya mjini zilizoshika nafasi za juu katika ligi hiyo mwaka jana huku akisisitiza kuwa bingwa wa mkoa katika msimu uliopita timu ya Tenenda imeshushwa daraja baada ya kusambaratika ilipotoka kuuwakilisha mkoa katika ngazi ya kanda.

No comments:

Post a Comment