Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, January 4, 2013

WAWILI WAUAWA KIKATILI MBEYA

WATU wawili wameuawa katika matukio mawili tofauti likiwemo na mkee kuuawa kwa kukatwa mapanga na mumewe akimtuhumu kuwa mshirikina.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwani athuman amemtaja Marehemu katika tukio hilo kuwa ni Lena Mbughi(34) huku mtuhumiwa wa mauaji hayo amabye ni mume wa marehemu akitajwa kwa jina la Israel Kayuni. Kamanda Athumani alisema mwili wa marehemu Lena ulikutwa chumbani kwake katika kitongoji cha Sambandolo kijijini Ipapa kata ya Ipunga wilayani Mbozi mnamo Januari 3 mwaka huu majira ya saa nane za mchana. Alisema karibu na mwili huo kulikutwa panga na damu ambapo inasemekana mume ambaye alikimbia mara baada ya mauaji alimvizia mkewe aliyekuwa amejipumzisha katika mkeka na kumtendea unyama huo. Inasemekana kuwa kwa muda mrefu Kayuni alikuwa akimtuhumu mkewe lena kuawa anajihusisha na vitendo vya kishirikina na ndiyo sababu ya kuchukua uamuzi huo usiofaa kwani alipaswa kutumia njia za mazungumzo na si kujichukulia sheria mikononi. Katika tukio jingine dreva Taksi aliyefahamika kwa jina la Emanuel Mbembela(30) mkazi wa mtaa wa Sogea katika mji mdogo wa Tunduma wilayani Momba amekutwa akiwa ameuawa na watu wasiofahamika na mwili wake kutupwa kichakani. Kamanda Athumani alisema mwili wa Emmanuel alikutwa Januari 2 mwaka huu majira ya saa 12:30 jioni kaika kichaka kilichopo jirani na Reli ya Tazara eneo la kijiji cha Mlowo barabara ya Mlowo Kamsamba. Alisema awali gari ya dreva tax huyo aina ya Toyota Spacio yenye namba T 381 BMT ilikodiwa na watu wasiofahamika na haikujulikana walimtaka awapeleke wapi hadi pale mwili wake ulipokuja kukutwa kichakani ukiwa na majeraha usoni na utosini. Kamanda Athumani alisema jeshi hilo linaendelea kuwasaka watuhumiwa wa matukio hayo yote na kuomba raia wema walio na taarifa za mahali walipo kulisaidia jeshi hilo.

No comments:

Post a Comment