Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, April 1, 2014

KIKONGWE ACHARANGWA NA SHOKA HADI KUFA AKITUHUMIWA UCHAWI

WATU watatu wamefariki dunia wilayani Chunya mkoani Mbeya katika matukio tofauti likiwamo la kikongwe aliyefahamika kwa jina la Belta Sanzia(68) mkazi wa kitongoji cha Maweni kijiji na kata ya Mkwajuni. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi amesema kikongwe huyo ameuawa akiwa numbani kwake kwa kukatwa na kitu kizito kinachodhaniwa kuwa ni shoka katika maeneo ya kichwani,mkono wa kulia na pia akatobolewa sehemu za ubavu wa kushoto tukio lililotokea usiku wa kuamkia jana(Machi 31). Kamanda Msangi amesema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina kwani marehemu aliyekuwa akiishi peke yake nyumbani kwake alikuwa akituhumiwa kuwaroga wanakijiji wenzake. Katika tukio la pili mzee aliyefahamika kwa jina la Luchagula Maenzeka(62) mkazi wa kitongoji cha Kininga kijijini Saza wilayani Chunya amekufa maji baada ya kuzidiwa na maji ya mto Saza uliopo kijijini hapo. Kamanda Msangi amesema tukio limetokea jana(Machi 31) saa 3:30 asubuhi katika kitongoji cha Kininga ambapo inadaiwa mzee huyo alishindwa kuyamudu maji ya mto huo alipokuwa akivuka kutoka upande mmoja kwenda mwingine huku akiwa amelewa pombe na ndipo akasombwa na maji. Tukio jingine ni la mtoto Julieth Christian mwenye umri wa miaka miwili mkazi wa kijiji cha Saza wilayani Chunya aliyekutwa amekufa maji ndani ya kisima kilichopo jirani na nyumba wanayoishi tukio lililotokea jana(Machi 31) saa 5:00 asubuhi.

No comments:

Post a Comment