Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, April 17, 2014

16 WATEULIWA KUENDELEA NA KIKOSI CHA MABORESHO YA TAIFA STARS

WACHEZAJI 16 wameteuliwa kubakia katika kikosi cha Maboresho ya timu ya Taifa(Taifa stars) huku wengine wawili wakipelekwa katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 20. Kocha msaidizi wa timu ya taifa Salum Mayanga alitangaza majina ya wachezaji wanaobaki katika kikosi hicho baada ya kufanyika kwa mchujo wa vijana hao walioanza kambi Machi 22 mwaka huu mjini Tukuyu wilayani Rungwe wakiwa 34. Mayanga aliwataja wachezaji hao kuwa ni pamoja na mlinda mlango Benedict Mlekwa kutoka Mara wakati walinzi wa kati ni Emma Simwanda kutoka kutoka mkoa maalumu wa kisoka Temeke na Joram Mgeveja kutoka Iringa. Walinzi wa pembeni ni Omari Kindamba kutoka Temeke, Edward Mayunga kutoka Kaskazini Pemba na Shirazy Sozigwa kutoka Ilala huku akiwataja viungo wa Ulinzi kuwa ni Yusufu Mlipili na Said Juma Ally kutoka Mjini Magharibi. Aliwataja viungo Washambuliaji kuwa ni Abubakar Ally Mohamed kutoka Kusini Unguja na Hashimu Ramadhani Magona kutoka Shinyanga, wakati Viungo wa pembeni ni Omari Athumani Nyenje kutoka Mtwara na Chunga Said Zito kutoka Manyara. Aliwataja washambuliaji kuwa ni pamoja na Mohammed Seif Said kutoka Kusini Pemba, Ayubu Kassim Lipati kutoka Ilala, Abdurahman Othman Ally kutoka Mjini Magharibi na Paul Michael Bundara kutoka Ilala. Kwa upande wa wachezaji wawili walioteuliwa kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya Miaka 20 aliwataja kuwa ni Mbwana Mshindo Musa kutoka Tanga na Bayaga Athanas Fabian kutoka Mbeya aliosema tayari wameungana na timu hiyo jijini Dar es salaam tayari kushiriki katika mechi za kirafiki za hivi karibuni. Hata hivyo Mayanga alisema kul;ikuwa na uwezekano wa kupatikana zaidi ya vijana hao kwani wachezaji walioachwa pia walikuwa na sifa na kuanzia sasa wachezaji hao wataendelea kuwa kwenye uangalizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) kwa kuwa mpango wa maboresho ya timu ya Taifa ni endelevu. Alisema wachezaji 16 walioteuliwa wanataraji kuondoka ijumaa hii kuelekea Dar es salaam kujiunga na kikosi cha Timu ya Taifa cha Awali kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya Kirafiki kisha watarudi tena wilayani Rungwe kwa ajili ya Kambi ya awamu ya Pili.

No comments:

Post a Comment