Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, April 4, 2014

PROF MWANDOSYA ATEULIWA KUWA MKUU WA CHUO KIKUU CHA MUST

CHUO kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya(MUST) kimepata viongozi wapya watakaokiongoza kufuatia uteuzi uliofanya na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na ofisi ya mahusiano ya MUST,Rais Kikwete amemteua Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Kazi maalum Prof.Mark Mwandosya(MB) kuwa Mkuu wa Chuo na kufuatiwa wakati Makamu Mkuu wa Chuo atabaki kuwa Prof. Joseph Msambichaka. Rais pia amemteua Prof. Osmund Kaunde kuwa Naibu mkuu wa chuo upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Chuo cha Sayansi Asili na Hisabati katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Prof. Emmanuel Luoga ameteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa Chuo wa Chuo hicho kwa upande wa Utawala, Fedha na Mipango wakati kabla ya uteuzi huo Prof Luoga alikuwa Mkuu wa Idara ya Upimaji wa Misitu katika Chuo Kikuu cha Sokoine. Chuo cha MUST kilipanda ambacho awali kilijulikana kama Chuo Cha Sayansi Na Teknolojia Mbeya(MUST) kilipandishwa hadhi ya kuwa chuo kikuu tangu mwaka 2012 na kilianza kutoa mafunzo kama chuo kikuu kuanzia mwaka wa masomo wa 2012/2013 katika fani mbalimabali ikiwemo shahada ya Usanifu Majengo, Uhandisi mitambo,Uhandisi Umeme na fani nyinginezo. Chuo hicho kimepata mafanikio makubwa sana katika utaoji wa wanafunzi wenye ujuzi wa hali ya juu katika fani mbalimbali hali inayotokana na upatikanaji wa maabara na vifaa vya kisasa vya kufundishia. Kwa mujibu wa ofisi ya Mahusiano Chuo pia kimefanikiwa kuunda vyuo ndani ya chuo hicho ikiwemo Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (College of Engineering and Technology), Taasisi ya Sayansi na Technolojia( Institute of science and Technology) na Shule ya biashara( School of Business).

No comments:

Post a Comment