Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, November 26, 2013

MWAKYEMBE AIFAGILIA PSPF

Waziri wa Uchukuzi Djk.Harrison Mwakyembe akisalimiana na wafanyakazi wa PSPF alipotembelea banda la mfuko huo kwenye maonesho ya biashara Mbeya(Mbeya Expo 2013)yanayoendelea katika viwanja vya kituo cha mikutano cha Mkapa jijini Mbeya. Afisa Uendeshaji wa PSPF Amina Mtingwa akitoa maelekezo ya namna ya kujiunga na Mpango wa uchangiaji kwa hiari mmoja wa wateja waliofika katika banda hilo.Mpango huo unawalenga watu wiote pasipokujali mhusika yuko katika sekta rasmi au isiyo rasmi. . Mhariri mkuu wa Lyamba Lya Mfipa Joachim Nyambo naye ni mmoja kati ya waliotembelea banda la PSPF na kupata maelezo juu ya namna ya kujiunga na pia faida za Mpango wa uchangiaji kwa hiari kama anavyoonekana hapa. WAZIRI wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe ameupongeza mfuko wa Penseni kwa watumishi wa umma (PSPF) akisema umekuwa na mchango mkubwa katika kuisaidia serikali kuwaletea maendeleo wananchi wake. Dkt Mwakyembe ameyasema hayo baada ya kutembelea banda la PSPF kwenye maonesho ya biashara yanayoendelea mkoani Mbeya yakiwashirikisha wafanyabiashara wa ndani na nchi jirani ya Kenya. Amesema kazi zinazofanywa namfuko huo ni nzuri na zenye tija inayojulikana kwa kila mmoja na kuwataka watendaji wa mfuko huo kuendelea kujituma kutekeleza majukumu yao ili sifa iliyopo iwe endelevu. Kwa upande wake afisa uendeshaji wa PSPF Bibi Amina Mtingwa amesema mfuko huo amesema kasi ya wananchi kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa hiari imeendelea kuongezeka ikilinganishwa na mwanzoni mwa mwaka huu ulipoanzishwa mpango huo. Hata hivyo Bi.Mtingwa amesema bado elimu zaidi inahitajika kwa jamii juu ya mpango huo aliosema una faida kubwa hasa kwa watu wanaojiwekea malengo ya kufanya jambo lolote lenye kuhitaji fedha kwakuwa mhusika ataweza kujikusanyia kwa kuweka kiasi kisichopungua shilingi 10,000 kwa kila mwezi.

No comments:

Post a Comment