Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, November 6, 2013

WAUAJI WAONDOKA NA KICHWA CHA MAREHEMU

Mwili wa mtu aliyeuawa kikatili kwa kukatwa kichwa ukiwa katika gari la polisi baada ya kufikishwa katika hospitali ya mkoa mjini Sumbawanga jana asubuhi kwa ajili ya kuhifadhiwa. Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka eneo la tukio mtu huyo alifanyiwa unyama huo nyakati za usiku wa kuamkia leo ambapo mwili wa mtu huyo ulitupwa kando ya daraja la mto katusa ambako pembeni yake kuna makaburi katika mtaa wa Tambazi katika Manispaa ya Sumbawanga. Mwenyekiti wa mtaa wa Tambazi, Christopher Kwimba alisema kuwa mtu huyo aliyeuawa anakadiriwa kuwa na umri katika ya miaka 25 na 27 hivyo ni vigumu kumtambua kwa haraka kutokana na wauaji kuondoka na kichwa chake.Baadhi ya askari polisi wakitelemsha maiti ya mtu ambaye ameuawa kwa kukatwa kichwa na watu kutoweka na kichwa chake usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya kuhifadhi katika hchumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya mkoa iliyopo mjini Sumbawanga.HABARI NA PICHA KWA HISANI YA BLOGU YA PEMBEZONI KABISA

No comments:

Post a Comment