Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, November 19, 2013

SUMBAWANGA MABINGWA UMISAVUTA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI

MASHINDANO ya michezo kwa vyuo vya ualimu(UMISAVUTA) kanda ya nyanda za juu kusini umemalizika kwa Chuo cha ualimu Sumbawanga kuchukua ubingwa wa mchezo wa soka. Sumbawanga ilichukua ubingwa huo baada ya kuinyuka Chuo cha Mpuguso cha wilayani Rungwe goli 5-3 kwa mikwaju ya penati iliyopigwa mara baada ya dakika 90 za mchezo wa fainali kumalizika kwa timu hizo kutoka suluhu huku giza likisababisha kutoongezwa kwa dakika 30 nyingine. Katika mchezo wa Voleyball Tukuyu iliinyuka Tandala seti 3-0 huku mchezo wa netiboli Sumbawanga uikaibuka bingwa kwa kuinyuka Mpuguso. Akizungumzia mwenendo wa mashindano hayo tangu kuanza hadi kumalizika kwake.mratibu wa mashindano hayo Doroty Mhaiki ambaye pia ni mkuu wa chuo cha Mpuguso kilichopo Rungwe alitaja ushiriki mdogo wa vyuo kuwa ni changamoto inayopaswa kutafutiwa ufumbuzi. Alisema mikoa ya Rukwa,Mbeya,Iringa,Njombe na Ruvuma ina jumla ya vyuo 17 vya ualimu lakini ni vinane pekee vilivyoshiriki mashindano hayo kwa mwaka huu. Changamoto nyingine ni ufinyu wa bajeti,uhaba wa vifaa vya michezo na viwanja hali iliyosababisha baadhi ya michezo kutochezwa kabisa hususani mchezo wa kikapu na wa mkono. “Ufinyu wa muda nao ulikuwa kikazwa kingine.Wachezaji wamelazimika kucheza kila siku pasipo kupumzika.Kiafya si vizuri na huenda ikawaletea madhara hata baada ya kumalizika kwa mashindano hayo” alisema. Akifunga mashindano hayo,mkuu wa wilaya ya Rungwe Chrispin Meela aliwataka waratibu wa mashindano hayo kuanza kuyahusisha mashirika ya hifadhi za kijamii ili yaweze kuwadhamini na kupunguza ukali wa bajeti za mashindano. Meela alisema mashirika hayo ni rafiki na vyuo vinavyozalisha wafanyakazi watarajiwa hivyo urafiki huo unapaswa kuimarishwa kwa mashirika kudhamini mashindano kama hayo ambayo yanafaida kwa wanavyuo ambao ni wateja wa baadaye.

No comments:

Post a Comment