Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, November 1, 2013

BABU MBARONI KWA MAUAJI YA MJUKUU

JESHI la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikila Zenobi Lusale (65) Mkazi wa Kijiji cha Sibwesa Tarafa ya Karema Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kumuua mjukuu wake kwa kumpiga na fimbo kichwani baada ya kumtuhumu kumwibia debe moja la mahindi. Kwa mijibu wa Kaimu kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Joseph Shilinde tukio hilo lilitokea jana saa 11 jioni katika kitongoji cha Senta Magogo Kijiji cha Simbwesa Tarafa ya Karema Wilayani hapa. Kaimu kamanda Joseph Shilinde alimtaja aliyeuawa kwa kupigwa na fimbo kichwani na babu yake kuwa ni Stansilaus Joseph (15) Mkazi wa kijij hicho. Siku hiyo ya tukio mtuhumiwa Zenobi alikwenda kwa jirani kunywa pombe ya kienyeji aina ya komoni nyakati za mchana na kisha aliporejea nyumbani kwake ambako alikuwa akiishi na mjuukuu wake huyo na ndipo alipo mwita kwa lengo la kufanya nae mazungumzo. Kaimu Kamanda huyo alieleza kuwa wakati wakiwa kwenye maongezi ndipo mtuhumiwa alipoanza kumshutumu mjukuu wake kuwa kuna mahindi debe moja yameibiwa ndani na yeye marehemu ndiye aliyeiba mahindi hayo Marehemu baada ya kuambiwa hivyo alikataa kuwa yeye hajaiba mahindi hayo labda aliuza mwenyewe na amesahau kama alimuuzia mtu kwani yeye hana tabia ya wizi. Inaelezwa kuwa baada ya kuelezwa hivyo mtuhumiwa alianza kumshambulia mjukuu wake kwa fimbo kichwani ambapo alipiga mayowe na ya kuomba msaada na huku akimsihi babu yake asiendelee kumpiga lakini hakufanya hivyo aliendelea kumpa kichapo na ghafla alianguka na kufariki dunia papo hapo. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya upepelezi wa awali kukamilika.

No comments:

Post a Comment