Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, November 7, 2013

12 MBARONI KWA MAUAJI YA KUMZIKA MTU AKIWA HAI

WATU 12 akiwemo Mwenyekiti wa kijiji wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya wakituhumiwa kwa mauaji ya kumzika mtu akiwa hai. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwan Athuman alimtaja mwenyekiti anayeshikiliwa kuwa ni wa kijiji cha Mshewe aliyefahamika kwa jina la Julius Ngole(52). Kamanda Athuman mnamo Novemba 7 mwaka huu,majira ya saa 08:30 katika kijiji cha Mshewe, kata ya Mshewe , tarafa ya bonde la Usongwe wilaya ya Mbeya vijijini Mkoani hapa wakazi wa kijiji cha Mshewe walimuua Hanahela Mwakabana(80) mkazi wa kijiji hicho kwa kumfukia katika kaburi na kumzika akiwa hai. Kamanda huyo alisema wananchi walifanya tukio hilo wakiongozwa na mwenyekiti wa kijijiu chon a kubainisha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni ni imani za kishirikina ambapo wakazi hao walikuwa wakimtuhumu marehemu kumuua mtoto wake Juma Hanahela(48) fundi ushonaji mkazi kijijini hapo aliyefariki dunia Novemba 5, mwaka huu kwa maradhi ya kiharusi ambayo alianza kuugua Oktoba 29, Mwaka huu na kulazwa hospitali teule ya Ifisi. Lakini wakazi wa Mshewe hawakubaliani na matokeo kuwa mkazi mwenzao alifariki kwa ugonjwa huo na kumtuhumu baba mzazi kuwa ndiye aliyemlioga mwanane. Kamanda Athuman watuhumiwa baada ya kumaliza kuchimba kaburi walimwambia kikongwe huyo aingie ndani ya kaburi ili apime kama linatosha kumzika mwanaye wake ndipo walipomfukia, kisha kuchimba kaburi lingine pembeni na kumzika mtoto wake Juma Hanahela.Hili ndilo kaburi alimozikwa kikongwe Hanahela Mwakabana(80)ambaye wanakijiji wenzake walimzika akiwa hai wakimtuhumu kumuua kwa kumroga mtoto wake.

No comments:

Post a Comment