Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, December 11, 2014

SIKU YA KILELE CHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA ILIVYOFANA KATIKA KATA ZA ILEMBO NA MASOKO

 Safari ilianzia kijijini Ilembo zilipo ofisi za Mradi wa kupinga ukatili wa kijinsia(GBV) na ukatili dhidi ya watoto(VAC) unaoendeshwa katika kata za Ilembo na Masoko wilayani Mbeya na kanisa la Anglikana kupitia shirika la Watereed kwa ufadhili wa watu wa Marekani.
 Kituo cha kwanza kikawa kijijini Ilomba na waelimishajirika wa mradi wa GBV na VAC kuanza shughuli ya kusakata rumba wakifurahia kupokelewa na wenyeji kem kemu
 Wakazi wa kijiji cha Ilomba wakifuatilia matukio kwa karibu zaidi kabla ya kuanza kupewa elimu ya GBV na VAC.Ikiwa ni katika kuadhimisha kilele cha siku 16 za kupinga ukatili zenye Kaulimbiu ya Amka sasa Fichua Ukatili wa kijinsia kwa Afya ya Jamii


 Watoto hawa wakashiriki kilele hiki kwa mashindano ya kucheza muziki wa aina mbalimbali
 Ama hakika burudani hii ilimvutia kila aliyefika uwanjani hapa,hata aliyekuwa akila tunda kama mtoto huyu anayeonekana kushoto kwa picha hii hapa juu alijikuta anajisahau kutafuna,na kubakia akiangalia kilichokuwa kikiendelea
 Mama huyu licha ya kusakata pia rhumba akishirikiana na TOTs pia akapongezwa kwa kuwa na ukarimu wa kupokea wageni hususani kama hawa waliopeleka ujumbe wenye lengo la kuibadili jamii juu ya masuala ya ukatili na athari zake katika ustawi wa jamii
 Ukafika muda wa TOTs kujitambulisha kabla ya kuanza kutoa elimu kwa wananchi wa kijiji hiki.

 Ukawaidia wakati uleee wa kutoa ujumbe.Hapa wananchi wakihamasishwa kutoa taarifa pale inapobainika kwenye maeneo yao kunafanyika vitendo vya kikatili.

 Safari ikaendelea.Hapa ni katika kijiji cha shigamba II.Wakazi wako tayari kusikiliza ujumbe

 Huku nako tuliwakuta wakazi walio na uwezo wa kusakata muziki kama hawa
 



 Akina mama na akina baba wakaona washindane katika kuvuta kamba.Msindi ni nani hiyo siri ya Lyamba Lya Mfipa


 Mmoja wa waelimisharika akiwa anafanya mawasiliano na wakazi wa kijiji tutakachokwenda tukitokea hapa







Na sasa ni kuondoka kuelekea kijiji cha Italazya kumalizia kazi ya tuliyotumwa ya kufikisha ujumbe kwa wananchi.






No comments:

Post a Comment