Neema akiwaongoza wasaidizi wake kutumbuiza kwenye hafla ya uzinduzi wa albamu yake.
Mshereheshaji maarufu jijini Mbeya Beny Benjamini(Dauble B) akisherehesha katika hafla hiyo
Sehemu ya vipande vilivyopo katika Video ya nyimbo zilizopo katika albamu iliyozinduliwa ikionesha Neema anavyoimba kwa hisia.
Wadau waliojitokeza kumsindikiza Neema kwenye uzinduzi wakimiminika kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya
Neema akijiandaa kukabidhi moja ya nakala za albamu yake kwa mgeni rasmi
Mzee wa kanisa akizungumza neno kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua albamu.
HABARI KAMILI
WASANII wakongwe wa nyimbo za Injili nchini
wameaaswa kuwa na ushirikiano na wasanii wachanga ili kuwajengea msingi bora wa
kudumu katika utoaji wa huduma hiyo.
Ombi hilo lilitolewa jana na msaanii anayechipukia
katika muziki wa injili Neema Mwangalika wakati wa uzinduzi wa albamu yake ya
kwenze aliyoipa jina la Kila Jambo na Wakati.
Katika uzinduzi wa albamu hiyo uliofanyika kwenye
kanisa la Wapo Misheni International la Airpot jijini hapa Neema alisema
wasanii wachanga wanahitaji kwa kiasi kikubwa ushirikiano wa wakongwe.
Alisema kwa kuwepo kwa ushirikiano wa pamoja
kutawezesha sanaa ya muziki wa injili kuendelea kukua na kuwa na mvuto mkubwa
zaidi.
“Ni kweli wakongwe wanakuwa na uzoefu mkubwa katika
muziki huu.Lakini pia wasanii wanaochipukia nao wana mapya wanayoweza kuyaleta
na kuwasaidia wakongwe.Hivyo kuna haja ya pande zote kushirikiana kwa pamoja”
“Sasa tukiendelea kujiweka katika makundi mawili
tofauti.Wakongwe wakasema wabaki kama walivyo.Wachanga nao wakaachwa peke yao
ni changamoto nyingine katika muziki wetu” alisema Neema.
Hata hivyo Neema alisema hakuna sababu ya wasanii
wachanga kukatishwa tama na vikwazo wanavyowekewa na wakongwe badala yake
wanapaswa kuendelea kujipa moyo huku wakiongeza ubunifu katika utendaji kazi
wao.
Akizungumzia changamoto ya uandaaji wa muziki wa
Injili,msanii huyo alisema ukosefu wa mtaji wenye kutosheleza mahitaji ni
tatizo linalokwamisha wasanii wengi wanaochipukia.
Akizindua albamu ya Kila Jambo na Wakati,afisa mtendaji
wa kata ya Iziwa jijini Mbeya Amanyisye Sageme pamoja na kuahidi kiasi cha
shilingi 600,000 aliwataka wasanii wa nyimbo za injili kuzingatia maadili
yanayozingatiwa na vitabu vitakatifu.
Aliwataka wasanii pia kuhakikisha wanadumisha amani
na utulivu wan chi kupitia sanaa yao sambamba na kujitambua kama kioo cha jamii
chenye kutumainiwa katika kutoa mafundisho ya maadili mema.
Albamu ya Kila Jambo na wakati ina nyimbo Pigana nao
Bwana,Ninasifu Jina,Nataka niwe juu,Omba sana,Matendo yako,Mahali
nimefika,Umeweka wimbo na Nioshwe na wewe.
No comments:
Post a Comment