Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, December 27, 2014

ZIARA YA DK.MWAKYEMBE NA WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU MKOANI MBEYA SIKU YA 1

 Waziri wa Uchukuzi Dk.Harison Mwakyembe akitoa ufafanuazi kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu juu ya namna kiwanda cha kusaga kokoto cha Kongolo kilichopo Mswiswi wilayani Mbarali kinachomilikiwa na Shirika la reli la Tazara kinavyofanya kazi ya uzalishaji wa kokoto kwaajili ya kuimarishia miundombinu ya reli.Katikati ni mwenyekiti wa kamati ya bunge Prof.Juma Kapuya akifuatiwa na kaimu meneja wa mgodi kokoto Juma Mizambwa
 Msafara Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu na waziri wa Uchukuzi Dk.Harison Mwakyembe ukiangalia namna kokoto zinavyozalishwa katika mgodi wa kuzalishia kokoto wa Kongolo uliopo katika kijiji cha Mswiswi wilayani Mbarali.

 Hapa wajumbe wa kamati walishauri uongizi wa kmgodi kona uwezekano wa kukopa fedha ili kuboresha mitambo na kuongeza uzalishaji wa kokoto ili kutengeneza faida zaidi ya sasa.
 Baada ya kutoka katika mgodi wa kusaga kokoto,safari ikaendelea mpaka kilipo kiwanda cha kutengenezea mataluma ya Reli kwa kutumia saruji maalumu badala ya chuma.
 Kaimu meneja wa mgodi kokoto Juma Mizambwa akielezea namna mataluma ya reli yanavyotengenezwa kwa kutumia saruji na si chuma
 Mataluma ya Reli yaliyotengenezwa kwa kutumia saruji maalumu yakiendelea kukaushwa kabla ya kuondolewa kwenye mtambo wa kutengenezea.


Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiangalia mataluma ya reri yaliyotengenezwa kwa kutumia saruji ambayo ni mbadala wa mataluma ya chuma hali inayopunguza gharama za ununuzi na usafirishaji wa mataluma ya chuma kutoka nje ya nchi.Mataluma haya ya saruji yanazalishwa na Tazara katika kiwanda kilichopo Mswiswi wilayani Mbarali.




 Ziara ikaendelea kurejea jijini Mbeya hadi ilipo karakana ya Shirika la Reli ya Tanzania na Zambia(TAZARA) maeneo ya Iyunga kama inavyoonyesha hapa chini.
 Hapa wabunge walielezwa namna Tazara mkoa wa Tanzania ilivyodhamiria kufufua vichwa vya treni vilivyoharibika kutokana na ajali mbalimbali.Usishangae kusikia mkoa wa Tanzania,Tazara inaendeshwa katika mikoa miwili ambayo ni mkoa wa Tanzania na mkoa wa Zambia.
 Wabunge walishauri kuangaliwa upya kwa sheria ya uanzishwaji wa Tazara ili kupunguza migongano ya mara kwa mara ambayo imekuwa ikiibuka na kusababisha utendaji wa shirika hilo kuendelea kuzorota,hivyo kulifanya lisiwe na tija katika maendeleo ya uchumi wa taifa.Wamunge walisema ni muhimu sheria ikabadilishwa ili bajeti ya Tazara mkoa wa Tanzania iwe inapelekwa katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma.

 Hiki ni moja kati ya vichwa vya treni vitakavyojengwa upya na Tazara.

 MATUKIO YA SIKU YA PILI YA ZIARA YATAKUJIA KESHO AKSANTE KWA KUWA NASI

No comments:

Post a Comment