Naye mtafiti toka Taasisi ya Utafiri wa Kilimo katika kituo cha utafiki wa kilimo ya Mart Uyole Pia Urio akiwaasa wanafunzi wa kike kupenda masomo ya Sayansi
Wanafunzi
kutoka shule mbalimbali za sekondari za jijini Mbeya waliohudhuria
tamasha la kuhamasisha wanafunzi wa kike kujiunga na Mafunzo ya Ufundi
na Sayansi katika chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya(MUST)
wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa masuala ya sayansi
HAHABARI KAMILI
WAZAZI kutowajengea mazingira mazuri ya
kuwahamasisha watoto wao kuyapenda masomo ya Sayansi tangu wangali wadogo
kumetajwa kuwa moja ya sababu zinazochangia watoto wa kike kutoyapenda masomo
hayo.
Hayo yalibainishwa na wadau mbalimbali wa Masomo ya
Sayansi kwenye tamasha ya kuhamasisha vijana kujiunga na M,afunzo ya Ufundi na
Sayansi lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya(MUST).
Miongoni mwa wadau waliozungumzia changamoto za
Masomo ya Sayansi kwa wanafunzi wa kike ni walimu wa shule za sekondari ambao
walisema jamii hususani wazazi wamekuwa wakichangia watoto kutoyapenda masomo
hayo.
Mwalimu David Ngonyani kutoka shule ya sekondari ya Samora
Machel ya jijini Mbeya alisema watoto wa kike wanayaogopa masomo ya Sayansi
kutokana na uelewa mdogo waliojengewa kutoka kwenye familia zao kuwa ni magumu.
“Tangu mtoto anapokuwa nyumbani anajengewa uelewa
kisaikolojia kuwa masomo ya Sayansi ni magumu na hawayawezi.Na pia familia hizi
pia zinashiriki kuwapotosha watoto tangu wakiwa ni wadogo kuwa upatikanaji wa
ajira kwa waliosoma sayansi ni mgumu ikilinganishwa na waliosoma sanaa” alisema
mwalimu Ngonyani.
Naye Mwalimu Vaileth Msigwa wa sekondari ya
Mwakibete alisema saikolojia ya kuyaogopa masomo ya sayansi inajengwa kwa
wanafunzi tangu shule ya msingi hadi sekondari.
Kwa upande wake Mwalimu Helena Masalu kutoka shule
ya sekondari ya Samora Macheri alisema wazazi wanapaswa kuwajibika kwa
kuwavutia watito wao kuyapenda masomo ya sayansi tangu wangali wadogo kwa
kuwaambia ukweli juu ya faida za kusoma masomo hayo.
Aawali Kaimu Makamu mkuu wa chuo cha Must Prof
Emanuel Luoga alisema jittihada zinazofanywa na wadau mbalimbali wa masuala ya
Sayansi ndani na nje ya nchi zimesaidia kuongezeka kwa udahili wa wanafunzi wa
wa kike chuoni hapo.
Naye mtafiti toka Taasisi ya Utafiri wa Kilimo
katika kituo cha utafiki wa kilimo ya Mart Uyole Pia Urio aliwataka wadau
kuendelea kuhimiza wanafunzi wa kike kusoma masomo ya sayansi ili kuwezesha
taifa kuondokana na changamoto ya uhaba wa wanasayansi.
No comments:
Post a Comment