Mkurugenzi
mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba akitoa taarifa yaa mikakati ya shirika hilo ili kukomesha tatizo la mgawo wa umeme nchini
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dk.Norman Sigalla akizungumza na maafisa wa Tanesco kabla ya kufungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa shirika hilo.
Afisa Mwandamizi wa Tanesco kanda ya Nyanda za juu kusini Salome Kondola akitoa neno la shukrani mara baada ya hotuba ya mkuu wa wilaya
Maafisa wa Tanesco wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Mbeya Dk.Norman Sigalla baada ya kiongozi huyo kufungua mkutano wa baraza lao.
HABARI KAMILI
SHIRIKA
la Ugavi la Umeme nchini(Tanesco) limesema ifikapo mwishoni mwa mwaka 2016
Tanzania suala la mgawo wa umeme litabaki kuwa historia.
Uhakika
huo unakuja kufuatia mikakati ya utekelezaji wa miradi ikiwemo Kinyerezi namba
moja wa megawati 150 ambao hadi sasa asilimia 90 ya utekelezaji wake
umekamilika.
Upo
pia mradi wa kinyerezi namba mbili wa megawati 240 ambao serikali iko kwenye
hatua za mwisho za maelewano ya kifedha baina ya wizara ya fedha,benki ya
Japani na benki ya maendeleo ya Afrika kusini ambapo ujenzi wa mradi huo
unatarajiwa kuanza mwakani.
Mkurugenzi
mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba ameyasema hayo wakati wa ufunguzi
wa mkutano wa Baraza kuu la 45 la wafanyakazi wa Tanesco linalofanyika jijini
Mbeya.
Mhandisi
Mramba amesema miradi ya kinyerezi namba tatu na nne imeanza kwa ubia kwa makampuni
mawili ya kichina na utekelezaji wake unatarajiwa kuanza mwakani kama ilivyo
kwa kinyerezi namba mbili.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Mbeya Dk.Norman Sigalla amewataka watoa huduma
kutoka shirika hilo kuwa na lugha zenye kumwelewesha mteja na si kujibu hovyo
hovyo.
Dk.Sigalla amesema
majibu mabovu ambayo yamekuwa yakitolewa na baadhi ya watendaji wa shirika hilo
yamekuwa yakisababisha serikali kulaumiwa na kuonekana haifai kwakuwa haiwathamini
wananchi katika kutoa huduma za nishati ya umeme.
Amesema
ni vema wataalamu hao wakawa na lugha zenye ukweli kwa wateja badala ya lugha
za kuwalaghai na kuwadanganya na mwisho wa siku mteja anakuja kubaini ukweli
uliopo na kulichukia shirika na serikali.
No comments:
Post a Comment