Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, December 14, 2014

MUDA WA KUPIGA KURA WAMALIZIKA KWA AMANI NA UTULIVU MBEYA


UCHAGUZI wa serikali za mitaa kwa mkoani Mbeya mpaka muda wa kupiga kura unamalizika hali imekuwa shwari na zoezi limekwenda kwa amani na utulivu.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi ameiambia Lyamba Lya Mfipa kuwa mpaka muda wa kumaliza zoezi la kupiga kura hakuna vurugu zozote zilizokuwa zimeripotiwa.

Kamanda Msangi amesema awali yalikuwepo mapungufu madogo madogo katika baadhi ya vituo ikiwemo kukosewa kwa fomu ambapo baadhi zilionekana kuwa na majina ya wagombea yasiyoendana na nembo za vyama vyao.

Amesema pia kuna baadhi ya vituo wasimamizi na mawakala walichelewa kufika  hivyo kusababisha zoezi la upigaji kura kuchelewa kiasi lakini akasisitiza kuwa kasoro zote zilitafutiwa ufumbuzi kwa haraka na zoezi likaendelea.

No comments:

Post a Comment