Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, February 8, 2014

WANAWAKE WAUAWA NA WAUME ZAO KISA WIVU

WATU watatu wamefariki dunia mkoani Mbeya katika matukio tofauti yakiwemo ya wanawake wawili kuuawa na waume zao kutokana na wivu wa kimapenzi wilayani Chunya. Kwa mujibu wa kamanda wa Polisisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi,katika tukio la kwanza lililotokea Februari 6 mwaka huu majira ya saa moja asubuhi katika kijiji cha Shoga wilayani Chunya mwanamke aliyefahamika kwa jina la Agnes Daud (32) mkazi wa kijiji hicho alikutwa ameuawa na mume wake aliyefahamika kwa jina la moja la Thomas. Kamanda Msangi alisema mume huyo alimuua mkewe kwa kumkata koromeo kwa kutumia kisu na kuwa mwili wa marehemu ulikutwa katika kibanda walichokuwa wanaishi na mume wake katika kambi ya uchimbaji madini mali ya Isack Mambo. Alisema katika tukio la pili lililotokea siku hiyo hiyo majira ya saa 12 jioni huko katika kitongoji cha London wilayani Chunya mwanamke mwingine aliyefahamika kwa jina la Defroza Gidion (18) mkazi wa kijiji cha Isanzu aliuawa kwa kupigwa ngumi na mateke sehemu mbalimbali za mwili wake na mume wake aliyefahamika kwa jina la Juma Januari. Alisema tukio hilo lilitokea wakati marehemu akiwa nyumbani na kubainisha kuwa vyanzo vya mauaji hayo yote mawili ni wivu wa kimapenzi. Alisema watuhumiwa walikimbia mara baada ya tukio na juhudi za kuwatafuta zinaendelea ambapo kamanda huyo wa polisi mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali walipo watuhumiwa wa matukio hayo azitoe katika mamlaka husika ili wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake, vinginevyo wajisalimishe wenyewe. Wakati huo huo kamanda Msangi alisema mwendesha pikipiki ya abiria maarufu kama bodaboda aliyefahamika kwa jina la Oswald Ndunguru(26) mkazi wa Iganzo amekufa papo hapo amefariki dunia baada ya kugongwa na gari. Alisema tukio hilo lilitokea februari 7 mwaka huu saa 12:00 jioni katika maeneo ya Kilimo Uyole jijini Mbeya ambapo Oswald akiwa anaendesha boda boda yenye namba T 322 CTJ aina ya Shineray aligongwa na gari yenye namba T893 BPD aina ya Isuzu iliyokuwa ikiendeshwa Emanuel Nsolo(31) mkazi wa kijiji cha Kikondowilayani Mbeya. Licha ya dereva wa boda boda kupoteza maisha eneo la tukio pia aajali hiyo ilisababisha majeraha kwa abiria wa pikipiki aliyefahamika kwa jina la Getruda Mwakalobo (28) mkazi wa Iganzo aliyelazwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya ambapo chanzo cha ajali ni dereva wa gari kukatisha barabara bila kuchukua tahadhari

No comments:

Post a Comment