Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, February 16, 2014

SIMBA YAIPIKU YANGA MAPATO NYUMBANI KWA MBEYA CITY

MCHEZO wa Mbeya City na Simba uliochezwa jumamosi katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya umeingiza jumla ya shilingi 125 milioni. Akitangaza mapatona ya kiingilio cha mchezo huo na mgawanyo wake,mwenyekiti wa Chama cha soka mkoani Mbeya(MREFA) Eliasi Mwanjala alisema kiasi hicho cha pesa kimetokana na watazamaji 21,000 walioingia kushuhudia mchezo huo kwa kiingilio sha shilingi 5000 kila mmoja. Kwa mapato hayo,mchezo wa Mbeya City na Simba umeingiza kiasi kikubwa cha fedha ikilinganishwa na kile kilichovunwa wakati Mbeya City walipochezaa na timu ya Yanga katika uwanja huo ambapo zilipatikanaN shilingi milioni 100 kiingilio kikiwa ni shilingi 5000 pia kwa kila mtazamaji aliyeingia uwanjani. Akizungumzia mgawo wa mapato ya mchezo huo,Mwanjala alisema shilingi 16,016,000 sawa na asilimia 18 ya fedha zote zilitolewa kwaajili ya kodi ya ongezeko la thamani yaani VAT na kiasi kilichosalia kugawanywa kwa kila timu kupata shilingi 25,316000 sawa na asilimia 29.5. Alisema shilingi 12,872,000 sawa na asilimia 15 zilikwenda kwa wamiliki wa uwanja,gharama za mechi shilingi 7,723,000 sawa na asilimia tisa,kamati ya ligi 7,723,000 sawa na asilimia tisa pia,mfuko wa maendeleo ya soka 3,861,000 huku Chama cha soka mkoa kikiambulia shilingi 3,003,000. Wakati Mrefa ikitangaza mapato hayo,kwa upande mwingine wadau wa soka mkoani hapa wamelalamikia ubadhirifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya viongozi wa kutumia vikundi vya watu kuuza tiketi bandia na wao kuzipitisha kama tiketi halali wawapo milangoni. Meneja wa uwanja wa Sokoine Modesrtus Mwaluka hakusita kulitupia lawama shirikisho la soka nchini (TFF) akisema lina baadhi ya watendaji wabadhirifu ambao wamekuwa wakitumia mechi kubwa kujinufaisha kwa kuwapa jukumu la kuuza tiketi bandia vijana wanaotoka nao Dra es salaam maarufu kama makomandoo kuja nao mikoani. Mwaluka alitolea mfano katika mechi ya Mbeya City na Simba akisema zilikamatwa tiketi nyingi bandia lakini baadhi yawasimamizi milangoni kutoa TFF walionekana kuziruhusu tiketi hizo wakidai zilikuwa halali hali iliyoleta migongano katika milango ya dimba la Sokoine.

No comments:

Post a Comment