Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, February 8, 2014

VIJANA MATATANI KWA NOTI BANDIA

POLISI mkoani hapa inawashikilia vijana wawili kwa tuhuma za kukutwa na noto bandia zenye thamani ya jumla ya shilingi 285,000. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi aliwataja vijana wanaoshikiliwa kuwa ni Patrick Msigwa (34) na Anthony Mwakifwamba (32) wote wakazi wa kijiji cha Isyonje wilayani Mbeya. Kamanda Msangi alisema vijana hao walikamatwa februari 7 mwaka huu saa 9:30 alasiri katika kijiji cha Simambwe kilichopo wilayani Mbeya wakiwa na noti bandia 57 zenye thamani ya shilingi 5000 kila moja. Alisema wakazi wa kijiji cha Simambwe ndio waliowakamata vijana hao walipokuwa wakinunua ships na kutoa noti bandia ya shilingi 5000 na walipobanwa ndipo walipoonesha noti nyingine. Kamanda Msangi alisema taratibu za kuwafikisha vijanahao mahakamani zinaendelea na kutoa rai kwa wananchi kuwa makini kwa kukagua noti wanazopewa wakati wa malipo ya aina yoyote ili kuepeka fedha hizo bandia.

No comments:

Post a Comment