Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, July 21, 2013

UZINDUZI GBV MKOA WA MBEYA KATIKA VIWANJA VYA LUANDA NZOVWE

Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro akihutubia mamia ya wakazi wa mkoa wa Mbeya waliohudhhuria uzinduzi wa mradi wa kupinga ukatili wa kijinsia na watoto(GBV) utakaoendeshwa kwa majaribio kwa mmuda wa miezi 18 kwenye baadhi ya maeneo ya wilaya sita zilizopo mkoani Mbeya Muuzaji wa Machungwa akiendelea kutoa huduma hiyo huku akiwa amepamba toroli la machungwa kwa kipeperushi chenye ujumbe wa kupinga ukatili wa kijinsia na watoto kwenye viwanja vya Ruandanzovywe ulikofanyika uzinduzi wa kupinga ukatili huo wa GBV.Mkurugenzi wa shireika la Watereed kanda ya nyanda za juu kusini Cmeron Garrette akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mbeya sehemu ya vifaa mbalimbali kwaajili ya wanawake wanaojifungua na watoto wachanga vyenye thamani ya shilingi milioni 300.Wa kwanza kulia ni mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya Seif Mhina.Vifaa hivyo vilivyotolewa na mfuko wa rais wa Marekani vilikabidhiwa juzi kwenye hafla ya uzinduzi wa kimkoa wa kupinga ukatili wa kijinsia na watoto(GBV) Mwenyekiti wa dawati la Jinsia na Watoto la Polisi mkoa wa Mbeya Mary Gumbo akisoma ripoti ya utendaji wa dawati hilo ambapo alisema kutokana na uelewa kuongezeka jamii imezidi kujitokeza kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia

No comments:

Post a Comment