Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, July 8, 2013

KANDORO AKANA KUPOKEA RUSHWA KUUGAWA MKOA WA MBEYA

MKUU wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ameonya baadhi ya watu wanaomtuhumu kupokea rushwa katika kupitisha maamuzi ya kuugawa mkoa wa Mbeya hali iliyopelekea kikao cha ushauri cha mkoa(RCC) kupitisha mapendekezo ya mkoa mpya kuitwa Songwe. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo(Julai 8),Kandoro amekiri kuzagaa kwa tetesi zinazomtuhumu kupokea rushwa ili apitishe mapendekezo ya kuundwa kwa mkoa mpya wenye kubeba wilaya za Ileje,Mbozi,Momba na Chunya wenye makao makuu Mkwajuni. Hata hivyo Kandoro amekanusha vikali kupokea rushwa na kusema wanaoeneza tuhuma hizo ni wachache walioshindwa kuwa na hoja za msingi ndani ya RCC katika kutetea upande waoo upewe mkoa mpya. Amesema maamuzi ya mapendekezo ya kuugawa mkoa wa Mbeya yalipitishwaza na RCC kwa kuzingatia maslahi ya umma na si mtu mmoja mmoja kama baadhi ya wajumbe walivyota. Tangu kupitishwa kwa mapendekezo ya Songwe kuwa mkoa mpya na kikao cha RCC wiki jana kumekuwa na mvutano mkali wa maneno kwa baadhi ya wananchi na viongozi huku pande kuu mbili zikionekana ni zile zilizotaka mkoa kuwa Rungwe na ule uliotaka kuwa Songwe.

No comments:

Post a Comment